Habari za Punde

*STARS YAICHAPA GAMBIA 2-1, YAPAA HADI NAFASI YA PILI KATIKA KUNDI C, YAIPUMULIA IVORY COAST

 Mshambuliaji wa timu ya Taifa 'Taifa Stars', John Boko (kushoto) akimtoka beki wa timu ya Taifa ya Gambia, wakati wa mchezo uliochezwa leo jioni katika uwanja wa Taifa. Katika mchezo huo Stars wameibuka kidedea kwa kuwachapa Gambia mabao 2-1. 
Gambia ndiyo waliokuwa wa kwanza kujipatia bao lililofungwa na mshambuliaji wake, MomodouCeesay, katika dakika ya 7 ya kipindi cha kwanza, huku mabao ya Stars, yakiwekwa kimiani na beki wake, Shamari Kapombe, katika dakika ya 60 na bao la pili likifungwa kwa mkwaju wa penati na Erasto Nyoni, katika dakika ya 84, baada ya mshambuliaji wa stars, Mbwana Samatta, kumlamba chenga ya maudhi beki wa Gambia na kuunawa mpira huo.

Kwa matokeo hayo sasa, Stars imefikisha jumla ya pointi 3 katika kundi C na kupaa hadi nafasi ya pili nyuma ya vinara wa kundi hilo, Ivory Coast, ambao wanaongoza kundi hilo wakiwa na Pointi 4,  baada ya mchezo wake wa jana kulazimishwa sare ya 1-1 na Morocco.
 Sehemu ya mashabiki wakiwa wamepoa jukwaani wakati Stars ilipokuwa nyuma kwa bao 1-0.
 Hata Raia wa kigeni walifika uwanjani kuishangilia Stars.
 Huyu naye pamoja na kuona kwa macho 'Live' mchezo huo lakini bado alikuwa na redio yake Booonge la Mkulima, akisikiliza matangazo ya mchezo huo uwanjani hapo.
Mashabiki wa Soka wa Stars, wakishangilia baada ya timu yao kupata bao la pili na la ushindi kwa mkwaju wa penati.

1 comment:

  1. "Hata Rais wa kigeni walifika uwanjani kuishangilia Stars."

    Kama uandishi wa habari wenyewe ndiyo huu basi kazi tunayo !!!

    ReplyDelete

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.