Kutoka uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, dakika 90 zimemalizika huku Timu ya Simba wakitoka vichwa chini baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Stand United, bao lililofungwa na mshambuliaji raia wa Nigeria, ambaye pia aliwahi kutamba na timu ya waandishi wa Habari Taswa fc, Abasirim Chidiebeze
katika dk ya 11 bao lililodumu hadi mwisho wa mwisho.
KIKOSI CHA STAND UTD
John Mwenda, Salehe Abdalah, Abuu Ubwa, Peter Mutabuzi, Jose Maganda, Reyna Mgungira, Pastory Athanas, Vitaris Mayanga, Abasirim Chidiebeze, Kheri Mohamed na Salum Kamana
KIKOSI CHA SIMBA
Ivo Mapunda, Mohamed Hussein, Murdish Juuko, Hassan Isihaka, Jonas Mkude, Ramadhan Singano, Abdi Banda, Elius Maguli, Ibrahim Hajibu, Hassan Kessy na Emmanuel Okwi.
Katika mchezo huo, Stand United walicheza pungufu katika dakika za mwisho baada ya wachezaji wake wawili Abuu Ubwa na Yassin Mustapha, kulimwa kadi nyekundu.
No comments:
Post a Comment