Habari za Punde

*YANGA YAONDOKA NA POINTI SITA NA MAGOLI SITA SOKOINE MBEYA

TIMU ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, leo imemalizia mchezo wake wa mwisho kati ya miwili iliyocheza kwenye uwanja wa Sokoine huko jijini Mbeya na kudhihirisha kauli yao waliyoitoka wiki iliyopita wakati wakiondoka jijini Dar, waliyosema kuwa wanaenda jijini Mbeya kwa lengo la kujichukulia pointi sita, jambo ambalo wamelitimiza leo.

Yanga imeweza kuibuka na ushindi wa pili mfululizo katika uwanja huo kwa kuwachapa wababe wa jiji hilo Mbeya City jumla ya mabao 3-1.

Katika mchezo wake wa siku ya Alhamis Yanga waliichapa Tanzania Prisons mabao 3-0 na hivyo kuwafanya wababe hao wakiondo jijini humo na jumla ya mabao sita na pointi sita, zinazowafanya waendelee kujichimbia kileleni kwa tofauti ya pointi tano na wapinzani wao katika kinyang'anyiro hicho Azam Fc weny pointi 26, ambapo hata akifanikiwa kushinda katika mchezo wake na Tz Prisons bado atakuwa nyuma kwa pointi mbili, ambapo Yanga sasa wanapointi 31.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Simon Msuva katika Dk 18, kwa kichwa akiunganisha Krosi ya Haruna Niyonzima, bao la pili lilifungwa na Mrisho Ngassa, katika Dk ya 59, baada ya kumramba chenga kipa wa Mbeya City, David Burhan, akiitendea haki pasi ya beki wake wa kushoto, Oscar Joshua.

Bao la tatu lilifungwa na Amis Tambwe  katika Dk ya 78, kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona iliyopigwa na Haruna Niyonzima.

Mbeya City walipata bao la kufutia machozi katika Dk ya 68 kupitia kwa Peter Mapunda, aliyemchambua kipa wa Yanga Ally Mustafa Bartez, kwa kichwa akiunganisha krosi ya Deus Kaseke.

KIKOSI CHA MBEYA CITY
David Burhan, Richard Peter, Hassan Mwasapile, Christian Sembuli, Yohana Morris, Steven Mazanda, Abdallah Seif, Rafael Alfred, Paul Nonga, Pius Kaseke na Themi Felix.

KIKOSI CHA YANGA
Ally Mustapha- 1
Juma Abdull- 12
Oscar Joshua- 3
Nadir Haroub- 23
Kelvin Yondani- 5
Salum Telela- 2
Simon Msuva- 27
Haruna Niyonzima- 8
Amiss Tambwe- 19
Mrisho Ngassa- 17
Andrey Coutinho- 7

BENCHI LA AKIBA.
Deo Munish- 30
Edward Charles- 28
Hassan Dilunga- 26
Danny Mrwanda- 24
Kpah sherman- 9
Saidi juma- 22
Rajab zahir- 4

KWA MATUKIO YA PICHA ZA MTANANGE HUU KAA NASI HAPO BAADAYE.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.