Habari za Punde

*MATUKIO KATIKA PICHA MTANANGE WA MBY CITY NA YANGA SOKOINE

 Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuba (katikati) akiigiza kumwamulia ugomvi mshambuliaji mwenzake, Mrisho Ngassa  wakati akiigiza kupigana na mchezaji mwenzake wa Yanga, ambaye leo alikuwa hayupo hata kwenye orodha ya Sub  Jerry Tegete, wakati Ngassa alipokuwa akishangilia bao lake la pili alilofunga katika dakika ya 59. 
Mbali na stailiyo mpya pia leo Ngassa aliweza kutoa staili nyingine mpya ambapo baada ya Amis Tambwe kutupia msumari wa tatu, alimnyang'anya note book na peni mwandishi aliyekuwa karibu na kuanza kuigiza kama anamhoki Amis Tambwe, huku Tambwe akionekana kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa.
 Mshambuliaji wa Yanga Simon Msuva, akijaribu kupenya msitu wa mabeki wa Mbeya City wakati wa mchezo huo.
 Sehemu ya mashabiki wa Yanga waliojitokeza kushuhudia mtanange huo.
 Kikosi cha kwanza cha Mbeya City.
Kikosi cha kwanza cha Yanga.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.