Habari za Punde

*MATUKIO KATIKA PICHA MTANANGE WA STAND UTD VS SIMBA HUKO SHINYANGA

 Mshambuliaji wa Simba Elius Maguri (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Stand Untd Peter Mutabuzi, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Ccm Kambarage, mjini Shinyanga. Katika mchezo huo Stand Untd, ilishinda bao 1-0.
 Mshambuliaji wa Simba Simon Sserunkuma (kushoto) akiwania mpira na beki wa Stand Untd Josend Maganda, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa leo jioni kwenye uwanja wa Ccm Kambarage mjini Shinyanga.
 Baadhi ya mashabiki wa Stand Utd, wakiingia uwanjani kwa mbwembwe.
 Wachezaji wa Stand Utd, wakiomba dua kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
 Wachezaji wa Simba, wakiomba dua kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
 Bango la mashabiki wa Stand Utd.
 Mashabiki wa Stand Utd, wakishangilia ushindi wa timu yao baada ya mchezo huo kumalizika.
 Timu ya Simba, leo wameshindwa kutamba mbele ya watoto wa Shinyanga na kutoka vichwa chini baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Stand United, bao lililofungwa na mshambuliaji raia wa Nigeria, ambaye pia aliwahi kutamba na timu ya waandishi wa Habari Taswa fc, Abasirim Chidiebeze
katika dk ya 11 bao lililodumu hadi mwisho wa mwisho.

KIKOSI CHA STAND UTD
John Mwenda, Salehe Abdalah, Abuu Ubwa, Peter Mutabuzi, Jose Maganda, Reyna Mgungira, Pastory Athanas, Vitaris Mayanga, Abasirim Chidiebeze, Kheri Mohamed na Salum Kamana

KIKOSI CHA SIMBA
Ivo Mapunda, Mohamed Hussein, Murdish Juuko, Hassan Isihaka, Jonas Mkude, Ramadhan Singano, Abdi Banda, Elius Maguli, Ibrahim Hajibu, Hassan Kessy na Emmanuel Okwi.

Katika mchezo huo, Stand United walicheza pungufu katika dakika za mwisho baada ya wachezaji wake wawili Abuu Ubwa na Yassin Mustapha, kulimwa kadi nyekundu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.