Habari za Punde

*WANANCHI ILULA WAZUA TAFRANI, WAVUNJA VIOO VYA BASI WAKIMTAFUTA POLISI BAADA YA KUZUILIWA KUFUNGUA BAA YA POMBE YA KIENYEJI ASUBUHI

 Habari zilizopatikana lutoka huko Ilula mkoani Iringa, zinasema kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa katika vurugu baina ya Askari Polisi na wananchi, zilizotokea leo asubuhi baada ya askari kufika katika eneo ilipokuwa imefunguliwa baa ya pombe za kienyeji kabla ya muda yaani muda wa kazi na askari hao kutaka kuwakamata wanywaji na wauzaji, jambo lililozua vurugu.

Katika vurugu hizo askari walionekana kuzidiwa nguvu na raia na mmoja wao katika kukimbia ili kujiokoa aliamua kukimbilia ndani ya basi la abiria la Nyagawa na ndipo raia hao walipoamua kulishambulia basi hilo kwa mawe na kuvunja vioo na wengine kuvamia kituo cha polisi na kuchoma moto na kisha kuchoma magari ya polisi.

Katika vurugu hizo imlzwa kuwa mwanamk mmoja alifariki dunia, na baadhi ya raia kujruhiwa.
Hii ni kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo huko Ilula.
 Moja ya gari lililochomwa moto katikati ya barabara.
 Baadhi ya raia wakishuhudia tukio hilo
Basi hilo lililovunjwa vioo na wananchi hao.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.