Habari za Punde

*FULL MKANDA CCM IKIMTAMBULISHA MGOMBEA WAKE MJINI DODOMA

 Mgombea Urais wa CCM Dkt. John Magufuli, akisalimiana na wananchi waliojitokeza kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo jioni kwa ajili ya kuhudhuria mkutano maalum wa kumtambulisha baada ya kuteuliwa na Chama chake cha CCM kuiwakilisha na kupeperusha Bendera yao katika uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akipiga gitaa la Bass wakati bendi ya Vijana Jazz, ilipokuwa ikitoa burudani jukwaani kwenye mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika leo mchana kwenye Ukumbi Mpya wa Dodoma Convetion Centre.
 Msanii Dokii na wanenguaji wake wakishambulia jukwaa wakati wakitoa burudani kwenye Mkutano huo leo mchana.
 Dokii na wanenguaji wake wakishambulia jukwaa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Waziri wake, Samiah Suluhu, baada ya kutangazwa kuwa mgombea Mwenza wa magufuli katika uchaguzi mkuu wa CCM mwaka huu.
 Sehemu ya umati wa Wanachama wa CCM waliohudhuria mkutano huo.
 Mama Tunu Pinda, akimpongeza Mgombea Mwenza, Samiah Suluhu..
 Mwenyekiti wa CCM Jakaya Kikwete akifanya mawasiliano wakati wa mkutano huo....
 Samiah Suluhu, akipongezwa na wenzake jukwaani.....
 Wana CCM wakiserebuka wakati wa mkutano huo, bendi ya TOT ilipokuwa ikitoa burudani.,
 Magufuli, akipongezwa na Pius Msekwa.....
 Mbunge wa Viti Maalum Singida, Martha Mlatta, akiwaongoza wenzake wa mkoa wa Singida kuserebuka wakati wa mkutano huo.
 Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake wakiwatambulisha wagombea, Magufuli na Samiah.
 Mgombea Mwenza, Samiah Suluhu, akiwasili Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwa ajili ya kutambulishwa leo jioni...
 Viongozi meza kuu.....
 Sehemu ya wageni waalikwa kwenye hafla ya kuwatambulisha wagombea....
 Lazaro Nyalandu akiteta jambo na Mbunge wa Maswa, John Shibuda wakiwa katika hafla hiyo.
 Mgombea Mwenza, Samiah Suluhu, akizungumza na wananchi baada ya kutambulishwa.
 Sehemu ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo ya utambulisho wa wagombea...
 Mgombea, John Magufuli, akizungumza baada ya kutambulishwa...
 Mgombea John Magufuli, akitembea uwanjani hapo kusalimia wananchi baada ya kutambulishwa na kuzungumza machache.
 Mgombea John Magufuli, akitembea uwanjani hapo kusalimia wananchi baada ya kutambulishwa na kuzungumza machache.
Mgombea John Magufuli, akitembea uwanjani hapo kusalimia wananchi baada ya kutambulishwa na kuzungumza machache.
 Makamu wa Rais Dkt.Bilal, akiagana na Philip Mangula...
 Kwa umakini wa kisikiliza..
Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete akihutubia wakati akifunga rasmi mkutano mkuu wa CCM leo mchana.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.