Moja ya basi liendalo kasi likiwa katika Kituo cha Shekilango likipakia na kushusha abiria, ambapo leo mabasi hayo yameanza rasmi kutoza nauli. Changamoto kubwa zilizopo katika usafiri huo leo ni pamoja na baadhi ya vituo kukosa mashine za kukatishia tiketi, huku baadhi ya abiria wakilalamikia kukosa chenji katika baadhi ya vituo.
Hili ni moja kati ya mabasi hayo yanayofanya safari zake kuelekea Mbezi mwisho baada ya kufika Kimara mwisho na kuchepuka kuingia barabara ya kawaida na kuendelea na safari ili kuwarahishia abiria waishio maeneo ya Mbezi mwisho.
Hili likitokea Mbezi mwisho kuelekea Kimara hadi maeneo ya katikati ya jiji.
Baadhi ya abiria wakitelemka katika basi hilo.




No comments:
Post a Comment