Habari za Punde

*MWINYIMVUA WATAKA WATUMISHI WA UMMA KUZINGATIA MAADILI YA UTUMISHI

 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akisoma maelekezo kuhusu umuhimu wa kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma kwa wafanyakazi wa Ofisi yake jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2016 (hawapo pichani) wakati wa maadhimishi ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoadhimishi kila mwaka Barani Afrika Juni 16-23.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoadhimishwa ofisi hapo.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoadhimishwa ofisi hapo. PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
********************************************
Na. wandishi Wetu, Dar
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua amewataka Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu kuzingatia maadili na kanuni za Utumishi wa Umma wakati wa Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma.

Dkt. Mwinyimvua amesema hayo tarehe 22 Juni, 2016 Ofisini kwake Jiji Dar es salaam,  wakati ofisi yake ikiadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kila mwaka huadhimishwa Juni 16 – 23, 2016 Barani Afrika ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Uongozi wa Umma kwa Ukuaji Jumuishi: Kuelekea katika Afrika tunayoitaka”.

“Kila mtumishi wa umma anapaswa kuzingatia maadili na sheria za utumishi wa umma ambazo ndio nguzo ya kuimarisha utendaji kazi na kuimarisha misingi na maadili ya Umma” alisema Dkt. Mwinyimvua”.

Kuna sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002, maboresho ya Kanuni ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2009 na miongozo mbalimbali inayoelekeza namna na jinsi mtumishi wa umma anapaswa kuifuata.

“Nafahamu zipo changamoto nyingi ambazo zinawapata watumishi wa umma nataka niwahakikishie kwamba, serikali inazitambua na inazifanyia kazi hivyo nawasii tufanye kazi kwa bidii kwani tunatambua kauli mbiu ya Serikali ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli ya Hapa Kazi tu inabidi kuitekeleza kwa kufanya kazi na tuache kufanya kazi kwa mazoea”, alisisitiza Dkt. Mwinyimvua.

Tumie mda wenu kujisomea vitabu, Magazeti, Vijarida, vitawasaidia kujifunza na kupata maarifa tofauti ambayo yataweza kuwasaidia kuwa wabunifu katika sehemu zenu za kazi, elimu na maarifa inapatikana kwa kujisomea tujijengee mazingira hayo yatawasaidia kuwaongezea ufanisi wa kazi, alisema Dkt. Mwinyimvua.

Kwa mwaka huu maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanaadhimishwa na Wizara na Taasisi za Serikali kwa kukutana na watumishi wa umma na wadau mbalimbali kwa lengo la kupokea changamoto, maoni, ushauri ikiwa ni lengo la Serikali la kutaka kuboresha huduma kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.