Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhiana magari tisa yenye thamani ya Shillingi Millioni mia nane na kumi kutoka Shirika la ICAP Tanzania kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika nchi nzima kuanzia mwezi Septemba, 2016. Kushoto kwake ni Claud Kumalija mwakilishi wa katibu Mkuu wa Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Dkt. Fatuma Mrisho akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhiana magari tisa yenye thamani ya Shillingi Millioni mia nane na kumi kati ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Shirika la ICAP Tanzania kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika nchi nzima kuanzia mwezi Septemba, 2016. Kushoto kwake ni Claud Kumalija mwakilishi wa katibu Mkuu wa Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kulia kwake ni Dkt. Michelle Roland Mkurugenzi Mkaazi wa Taasisi ya Marekani ya Kudhibiti Magonjwa – (Centre for Disease Control and Prevention - CDC).
Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika wa Taasisi ya Marekani ya Kudhibiti Magonjwa – (Centre for Disease Control and Prevention - CDC) Dkt. Michelle Roland akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi magari tisa yenye thamani ya Shillingi Millioni mia nane na kumi kwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika nchi nzima kuanzia mwezi Septemba, 2016.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa pamoja na mwakilishi wa katibu Mkuu wa Wizara Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Claud Kumalija wakionyesha ufunguo wa gari mbele ya waandishi wa habari na wageni waalikwa kuashiria kupokea magari tisa yaliyotolewa na Shirika la ICAP Tanzania kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika nchi nzima kuanzia mwezi Septemba, 2016.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akiwasha gari kama ishara ya kupokea magari tisa yenye thamani ya Shillingi Millioni mia nane na kumi kutoka Shirika la ICAP Tanzania kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika nchi nzima kuanzia mwezi Septemba, 2016. Hafla ya makabidhiano ya magari hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (wa kwanza kulia) pamoja na wageni waliohudhuria katika hafla ya kukabidhiana magari wakiangalia baadhi ya magari yaliyotolewa na Shirika la ICAP Tanzania kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika nchi nzima kuanzia mwezi Septemba, 2016. Hafla ya makabidhiano ya magari hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA IMMANUEL GHULA
*******************************************
OFISI ya Taifa ya Takwimu imekabidhiwa magari tisa aina ya Land cruiser yenye thamani ya Dola za
kimarekani laki nne na elfu tano ($ 405,000) sawa na Shillingi za kitanzania Milioni
mia nane na kumi (810,000,000/=) kutoka Shirika lisilo la kiserikali la ICAP
linaloendeshwa na Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani kwa ajili ya Utafiti
wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utakaofanyika mwezi Septemba, 2016.
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhiana magari hayo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amelishukuru
Shirika la ICAP kwa msaada huo ambao utasaidia kupunguza gharama za kukodi
magari kwa ajili ya kufanyia utafiti.
“Napenda
kuchukua fursa hii kulishukuru Shirika la ICAP kwa kutupatia msaada huu wa
magari tisa yenye thamani ya Shillingi milioni mia nane na kumi. Huu sio msaada
mdogo kwani fedha ambazo zingetumika kukodisha magari ya utafiti, sasa
zitatumika katika shughuli nyingine za kimaendeleo,” amesema Dkt. Chuwa.
Amesema
katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), takwimu rasmi
zinahitajika ili kupima utekelezaji wake na hivyo utafiti huu utakapokamilika
utasaidia kutoa takwimu zitakazotumika kupima utekelezaji wa malengo hayo.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la ICAP Tanzania, Dkt. Fernando
Morales amesema utafiti huu unalenga kupima Viashiria na Matokeo ya UKIMWI nchini
ili kujua ni kwa kiwango gani Tanzania imepiga hatua katika kupambana na
ugonjwa huo.
Dkt.
Morales amesema msaada huu wa magari utasaidia kurahisisha usafiri wa kutoka eneo
moja la utafiti hadi lingine na kuweza kusaidia katika upatikanaji wa taarifa
muhimu za utafiti huu.
Nae
Mkurugenzi Mkaazi wa Taasisi ya Marekani ya Kudhibiti Magonjwa – (Centre for
Disease Control and Prevention - CDC) Dkt. Michelle Roland amesema kutokana na
utafiti huu kufanyika kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya ukusanyaji wa
takwimu, kutasaidia kupunguza gharama ambazo zingetumika kama utafiti huu ungefanyika
kwa njia ya kutumia madodoso ya karatasi.
Ameongeza
kuwa utafiti huu utafanyika kwa kutumia sampuli wakilishi ya kaya zipatazo
15,800 Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, na kuwafikia walengwa wapatao elfu
arobaini (40,000) wakiwemo watoto wasiopungua elfu nane (8,000).
Matokeo
yanayotarajiwa kupatikana katika utafiti huo ni pamoja na taarifa sahihi kuhusu
hali ya maambukizi mapya ya VVU, upatikanaji wa huduma za tiba na matunzo kwa
watu wanaoishi na VVU hapa nchini na kutambua ni kwa kiwango gani huduma hizi
zimesaidia katika kuudhibiti ugonjwa wa UKIMWI.
Utafiti
huu wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania utafanywa kwa pamoja na Shirika
la ICAP Tanzania, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
kwa Tanzania Bara, Wizara ya Afya kwa Tanzania Zanzibar, Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS), Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar (OCGS), Tume ya
Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) na Tume ya UKIMWI Zanzibar (ZAC).
No comments:
Post a Comment