Habari za Punde

*SERIKALI YATENGA TSH. BILIONI 5 KUJENGA JENGO LA MIONZI HOSPITALI YA RUFAA MKOANI MBEYA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akijadiliana jambo na Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA) mchungaji Mhe. Peter Msigwa wakati wa kikao cha asubuhi cha Bunge hilo linaloendelea mjini Dodoma.
 Wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Mount Meru ya Arusha pamoja na walimu wao wakifuatilia mjadala wa kikao cha mkutano wa Bunge mjini Dodoma.
 Wabunge wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma wakiendelea na msimamo wao wa kutombua Naibu Spika wa Bunge hilo, Dkt. Tulia Ackson.
 Mhe. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa akijibu maswali ya Wabunge asubuhi Bungeni Dodoma wakati wa maswali ya papo kwa papo kwa Mhe. Waziri Mkuu.
 Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mhe. Peter Serukamba (kulia) akijadiliana jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof Makame Mbarawa wakati wa kipindi cha asubuhi cha Bunge hilo mjini Dodoma.
 Mbunge wa (Viti Maalum) CCM Mkoa wa Pwani, Mhe. Zainab Vullu akiuliza swali kwa Waziri Mkuu Bungeni Mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akifafanua jambo kwa wabunge wakati wa kipindi cha asubuhi cha Bunge hilo mjini Dodoma.
Mbunge wa Mwibara (CCM), Mhe. Kangi Lugola akiuliza swali Bungeni mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Mawaziri wa Serikali kutoka kushoto, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo (Nishati na Madini), Mhe. William Lukuvi (Ardhi, Nyumba, na Maendeleo ya Makazi) na Mhe. Charles Mwijage (Viwanda, Biashara na Uwekezaji) wakijadiliana jambo ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Jonas Kamaleki, Maelezo - Dodoma
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 5 katika mwaka 2016/17 zitazotumika kwa ajili ya ujenzi wa jengo la X-Ray katika hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya.

Hayo yalisemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi aliyetaka kujua lini jengo la Maabara ya Mionzi linalojengwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mbeya litakamilika.

Ummy alisema katika mwaka wa Fedha 2015/16  Tsh. Bilioni 8 zilitengwa kwa ajili ya ujenzi huo, ingawa ujenzi huo haukufanyika lakini nia ya Serikali ya kukamilisha ujenzi wa jengo hilo uko pale pale.

Akiainisha matumizi ya pesa zilizotengwa kwa mwaka wa Fedha 2016/17, Ummy alisema Tsh. Bilioni 3 zitatumika kuendeleza ujenzi pamoja na kulipa deni lililobaki kwa mkandarasi aliyekuwa anajenga na bilioni 2 zitatumika kununua vifaa tiba vikiwemo CT- Scanner na MRI.

Akijibu swali la nyongeza toka kwa Mhe. Catherine Majige (Viti Maalum CCM), Mkoa wa Arusha, Ummy alisema bilioni 9 zimetengwa kwa ajili mya kununua vifaa tiba ikiwemo kuweka CT-Scanner na MRI katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru.
Aidha Waziri Ummy alisema kuwa Wizara imepata kibali cha kuajiri wafanyakazi 10,000 wa afya nchini kati ya maombi ya kuajiri wafanyakazi 30,000.

Aliongeza kuwa Serikali imetenga bajeti kwa mwaka wa Fedha 2016/17 kwa ajili ya kuboresha Hospitali za rufaa nchini ikiwemo ya Singida, Sekou Toure ya Mwanza, Mbeya na Arusha.

Ummy alisisitiza kuwa ni nia ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuboresha sekta ya afya  nchini na kuwafanya wananchi kuwa na afya bora.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.