"TATU MZUKA kwa ushirikiano na Naibu Waziri, Kazi, Ajira na Vijana Mh. Anthony Mavunde (Mbunge Dodoma Mjini) wakikabidhi matofali 3000 na mifuko 100 ya saruji kwa mmoja wa viongozi katika kata ya Makutupora kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi Mpya za Muungano na Mbande. Kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili kila moja.
**************************
Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Antony Mavunde mwishoni mwa wiki amekabidhi matofali 3000 na mifuko ya saruji 100 katika Kata ya Makutupora kwa ajili ya kuanza awamu ya kwanza ya ujenzi wa Shule za Msingi Mpya za Mbande na Muungano Wilaya ya Dodoma mjini mkoani Dodoma.
Msaada huo alioukabidhi umetoka kwa kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Tatumzuka ambayo ilikabidhi zawadi kwa washindi katika droo ya michezo hiyo,Mavunde aliishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo na kuwaomba wadau wengine kujitokeza zaidi ili kusaidia kuboresha Elimu nchini.
Waziri Mavunde alisema kuwa ujenzi wa shule hizo utasaidia kupunguza adha inayowapata wanafunzi kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilomita 7 kufuata shule katika eneo la Veyula.
"TATU MZUKA kwa ushirikiano na Naibu Waziri, Kazi, Ajira na Vijana Mh. Anthony Mavunde (Mbunge Dodoma Mjini) wakiwashukuru baadhi ya wakazi na viongozi mbalimbali wa kata ya Makutopora mara baada ya kukabidhi matofali 3000 na mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi Mpya za Muungano na Mbande.Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma.
Baadhi ya Wananchi mbalimbali waliojitokeza kutoka kijiji cha Makutopora na Mbande kushuhudia tukio la makabidhiano ya matofali 3000 na mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi Mpya za Muungano na Mbande,iliyotolewa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Tatumzuka ikishirikiana na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Antony Mavunde.
No comments:
Post a Comment