NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MKUU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, (pichani juu), ameongoza mahafali ya kumi (10), ya Chuo kikuu kishiriki cha Elimu (DUCE) cha Chuo kikuu Dar es salaam kwenye viwanja vya chuo hicho, Chang’ombe jijini Dar es Salaam leo Novemba 15, 2017.
Katika mahafali hayo zaidi ya wanachuo 1,443 waliochukua mafunzo ya Shahada ya Elimu ya Jamii na Elimu, (BAED), Shahada ya Elimu ya Sayansi na Elimu, (Bsc) na Shahada ya Elimu (BED), pamoja na wahitimu waliojiendeleza (Post graduate),
walitunukiwa shahada ya kwanza, ambapo mwanachuo Dadi Omary Safari, alipewa tuzo ya kuwa mwanachuo bora zaidi kitaaluma.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, akimpongeza mmoja wa wahitimu wa Shahada ya Elimu ya Jamii na Elimu, (BAED) Amisa Hassan.
Baadhi ya wahitimu katika mahafali ya 10 ya ya Chuo kikuu kishiriki cha Elimu (DUCE) cha Chuo kikuu Dar es salaamwakiwa kwenye mahafali hayo.
Furahaya kuhitimu na kutunukiwa shahada.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, akisoma hotuba yake.
Dkt. Kikwete, akipitia ratiba ya mahafali hayo.
Dkt. Kikwete akitangaza kuwatunuku shahada baadhi ya wanachuo hao.
Mwanachho bora kitaaluma Dadi Emmanuel Safari akiwa na tuzo yake.
Dkt. Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa wahitimu, Amisa Hassan, na baba mdogo wa muhitimu huyo, Khalfan Said.
No comments:
Post a Comment