MISS Tanzania 2008, Nasreen Kareem, akipanga bidhaa zake katika banda la maonesho ya Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es salaam, kuelekea mkutano mkuu wa 39 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika ambapo jumla ya nchi 16 zinashiriki, Tanzania ikiwa ni mwenyeji huku Rais Dkt. John Pombe Magufuli akitarajia kukabidhiwa Uenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa muda wa mwaka mmoja..
Sehemu ya mabanda
MFANYAKAZI wa Kampuni ya Simu za mkononi Airtel Tanzania, Bernad Mbisamatole (katikati) akiwasajili wateja wa mtandao huo kwa alama za vidole 'Kieletroniki' katika banda la maonesho ya 4 wiki ya Viwanda kuelekea mkutano mkuu wa 39 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika SADC kwenye Viwanja vya Ukumbi wa Julius Nyerere Dar es Salaam. Serikali ilitangaza mwisho wa usajili wa Kielekitroniki ni mwezi Disemba mwaka huu.
OFISA Masoko wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC), Nassor Salum (kulia), akitoa maelezo kwa wananchi, kuhusu manukato asilia yatokanayo na mimea, wakati wa Maonyesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC, katika viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, leo.
MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, (TPDC), Dk.James Matarajio, akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo, wakati wa maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC katika Viwanja vya Ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, leo kuelekea Mkutano Mkuu wa Nchi Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika utakaoshirikisha jumla ya Nnchi 16 za Jumuiya hiyo unaoanza Agosti 9 kwa Mawaziri na kwa Marais utafanyika kwa siku mbili.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Atasha Products, Asha Kasililwa (kulia) akitoa maelezo ya matumizi ya unga wa Ubuyu kwa mwananchi aliyetembelea katika banda lake la maonesho ya nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za SADC yanayofanyika kwnye viwanja vya Ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, kuelekea Mkutano mkuu wa 39 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika.
MENEJA wa Kitengo cha Bandari wa Wakala wa Vipimo, Peter Chuwa (kushoto) akifafanua jambo kwa wadau waliotembelea banda lao la maonesho ya nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za SADC yanayofanyika kwnye viwanja vya Ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, kuelekea Mkutano mkuu wa 39 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika SADC.
MSANII wa kuchora, Amani Grem, akiandaa sanaa yake ya Picha za Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alizochora kwa kutumia Shanga za rangi. Grem ni mshiriki katika maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC ukumbi wa Juulius Nyerere Dar es Salaam, ambapo jumla ya nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika zinashiriki.
WASANII wa kikundi cha Sanaa cha Jeshi la Wananchi JWTZ Mwenge, wakitoa burudani nje ya Ukumbi wa Julius Nyerere, wakati wa maonesho ya Nne ya Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) jijini Dar es salaam, kuelekea mkutano mkuu wa 39 wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo, ambapo jumla ya nchi 16 zinashiriki.
No comments:
Post a Comment