Habari za Punde

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN KUFUNGA MAONESHO YA WIKI YA VIWANDA KESHO

  MKURUGENZI wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko na Uhusiano Benki ya TIB Said Mkabakuli (wapili kushoto) wakati alipotembelea banda la maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC, katika viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, ambapo jumla ya nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika SADC zinashiriki katika maonesho hayo kuelekea Mkutano Mkuu wa 39 wa jumuiya hiyo unaotarajia kuanza Agosti 17 na kumalizika 18. Wa pili (kulia) ni Mkurugenzi wa Konnectt Wires and Cables, Sheila Mwapachu.
 MKURUGENZI wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzanite Founder Foundation, Asha Ngoma (kushoto) wakati alipotembelea banda la maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC, katika viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, ambapo jumla ya nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika SADC zinashiriki katika maonesho hayo kuelekea Mkutano Mkuu wa 39 wa jumuiya hiyo unaotarajia kuanza Agosti 17 na kumalizika 18. 
 MKURUGENZI wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC, katika viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, ambapo jumla ya nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika SADC zinashiriki katika maonesho hayo kuelekea Mkutano Mkuu wa 39 wa jumuiya hiyo unaotarajia kuanza Agosti 17 na kumalizika 18. 
************************************************
RAIS wa Zanzibar ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,  Dk. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kufunga maonesho ya  Viwanda vya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC).
Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo,Dk.Hasani Abasi amesema baada ya maonesho hayo kufungwa wageni waliohudhuria watapata nafasi ya kutembelea maeneo ya viwanda ili kuangalia utekelezaji wake kwa vitendo.
“Katika ufungaji Dk.Shein atafunga majira ya mchana na huku  kesho kutwa baadhi ya wageni watapata fursa ya kutembelea  viwanda kwa ajili ya kuangalia utekelezaji,”alisema
Alitaja maeneo ambayo wageni hao watatembelea kuwa ni Unguja,Kibaha, Bagamoyo kwa ajili ya kuona Tanzania ilivyotekeleza kwa vitendo sera ya viwanda.
Pia Dk.Abasi alitoa ratiba ya mkutano huo baada ya kufungwa kesho kwamba kuanzia Agosti 9-12 kutakuwa na mkutano wa maofisa  waandamizi wa  nchi za SADC ambao ni makatibu wakuu.
Alisema katika mkutano huo Katibu Mkuu wa Wizara  ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,atakuwa Mwenyekiti na kujadili ajenda mbalimbali zilizopita. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Agosti 14, mwaka huu, kutakuwa na vikao vya mawazili wa nchi za SADC ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Profesa Palamagamba Kabudi atakuwa akichukua nafasi ya Uenyekiti wa baraza la Mawazili kwa nchi.
Agosti 15, mwaka huu kutakuwa na majadiliano ya ushirikiano wa  kikanda ambapo Rais Mstaafu,  Benjamini Mkapa  akauongoza  na kuelezea uzoefu wake.
Dk.Abasi alisema majadiliano hayo yatafanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaammkwenye ukumbi wa maktaka  mpya ya Taifa .
“Kiongozi huyo ataeleza uzoefu wake wa ushiriki kikanda  na amekuwa akifahamu mambo mengi kuhusiana na SADC   ambapo Agosti 16, mwaka huu kutaundwa muundo wa  wa SADC wa masuala ya ulinzi na usalama,” alisema.
 Alisema katika mkutano huo  RaIS  Dk. John Magufuli na Rais Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete  watahudhuria.
 Vilevile alisema viongozi hao wataangalia  changamoto za ulinzi na usalama kwa nchi za SADC  na jinsi ya kuzisimamia.
Agosti 17  na 18 ndio utakapofanyika mkutano mkuu  wa wqakuu wa nchi na serikali katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere na Rais Dk. Magufuli anatarajia kuongoza mkutano huo baada ya kuidhinishwa kuwa mwenyekiti wa SADC kiwa kipindi cha mwaka mmoja
 Kwa upande mwingine, Dk. Abasi alisema kupitia maonyesho ya Viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika alichojifunza ni kuona nchi za jumuiya hiyo zikifanya vizuri  katika uzalishaji wa bidhaa za viwandani.
 “Moja ya fursa ya kunufaika na SADC ni kwenda kujua bidhaa zinazozalishwa nchi za jumuiya hiyo aidha mtu azitumie  kwa matumizi ya nyumbani au apate fursa ya nchi gani inahitaji bidhaa gani” alisema
 Akisikiliza maelezo kutoka kwa msemaji wa TRC Benny Mwanantala.
 Akipokea zawadi ya kitabu kutoka  kwa Mwanagiolojia...
 Majadiliano yakiendelea ndani ya Ukumbi huo.
 Washiriki wa majadiliano wakisikiliza kinachoendelea ukumbini humo.
  WANANCHI wakitembelea kujionea Bidhaa za Ngozi zinazozalishwa na Jeshi la Magereza katika banda la maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC, katika viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, ambapo jumla ya nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika SADC zinashiriki katika maonesho hayo kuelekea Mkutano Mkuu wa 39 wa jumuiya hiyo unaotarajia kuanza Agosti 17 na kumalizika 18.
  MKURUGENZI wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Kitengo cha Bandari Wakala wa Vipimo, Peter Chuwa (kulia) wakati alipotembelea banda la maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC, katika viwanja vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, ambapo jumla ya nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika SADC zinashiriki katika maonesho hayo kuelekea Mkutano Mkuu wa 39 wa jumuiya hiyo unaotarajia kuanza Agosti 17 na kumalizika 18.
 WASHIRIKI wa maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC, kutoka mataifa mbalimbali ya nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC, wakiwa katika majadiliano katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, ambapo jumla ya nchi 16 za Jumuiya hiyo zinashiriki kuelekea Mkutano Mkuu wa 39 wa jumuiya hiyo unaotarajia kuanza Agosti 17 na kumalizika 18. 
 MSANII wa Sanaa ya uchoraji 'Sine Art', Ester Nelson, akimalizia kuchora picha ya Mazingira nje ya Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Julius Nyerere dar es Salaam, aliposhiriki Maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC, ambapo jumla ya nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika SADC zinashiriki katika maonesho hayo kuelekea Mkutano Mkuu wa 39 wa jumuiya hiyo unaotarajia kuanza Agosti 17 na kumalizika 18. Kushoto ni Ofisa Habari na Mawasiliano Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Said Ameir na Mtakwimu Mwandamizi, Childa Hamis.
BAADHI ya washiriki wa majadiliano ya Maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC,  wakiwa katika foleni ya kuingia Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam, ambapo jumla ya nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika SADC zinashiriki katika maonesho hayo kuelekea Mkutano Mkuu wa 39 wa jumuiya hiyo unaotarajia kuanza Agosti 17 na kumalizika 18. Kushoto ni Ofisa Habari na Mawasiliano Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Said Ameir na Mtakwimu Mwandamizi, Childa Hamis.
*******************************
 KARIMJEE
 MTAKWIMU Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea Mabanda ya Maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC, katika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam, ambapo jumla ya nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika SADC zinashiriki katika maonesho hayo kuelekea Mkutano Mkuu wa 39 wa jumuiya hiyo unaotarajia kuanza Agosti 17 na kumalizika 18. Kushoto ni Ofisa Habari na Mawasiliano Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Said Ameir na Mtakwimu Mwandamizi, Childa Hamis.
 MKURUGENZI Mwenza wa Kampuni ya Saliss na Ambi General Enterprises, Said Ally na Ofisa Masoko, Veronica Lina, wakitoa maelekezo jinsi wanavyotengeneza Majani ya chai 'Tea Masala' kwa wateja wao waliotembelea Banda la Maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC, katika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam, ambapo jumla ya nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika SADC zinashiriki katika maonesho hayo kuelekea Mkutano Mkuu wa 39 wa jumuiya hiyo unaotarajia kuanza Agosti 17 na kumalizika 18. Kushoto ni Ofisa Habari na Mawasiliano Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Said Ameir na Mtakwimu Mwandamizi, Childa Hamis.
MTAKWIMU Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa, akimsikiliza Mjasiriamali, Magreth Kabonge wa Upendo Arts, wakati alipotembelea Mabanda ya Maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda ya SADC, katika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam, ambapo jumla ya nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika SADC zinashiriki katika maonesho hayo kuelekea Mkutano Mkuu wa 39 wa jumuiya hiyo unaotarajia kuanza Agosti 17 na kumalizika 18. Kushoto ni Ofisa Habari na Mawasiliano Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Said Ameir na Mtakwimu Mwandamizi, Childa Hamis.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.