Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Unga cha YES CPL kilichopo Kibaha, Zhang Jie
(kulia) akitoa maelezo kwa baadhi ya washiriki wa Maonesho ya Nne ya
Wiki ya Viwanda ya SADC, walipofanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho
kilichopo Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani juzi.
Wakitembelea kukagua jinsi unga unavyozalishwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo NDC, Prof. Damian Gabagambi, akipokea zawadi ya Kiroba cha Unga kutoka kwa Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Unga cha YES CPL, Zhang Jie kilichopo Wilaya ya Kibaha Mkoani pwani, baada ya kutembelea kiwanda hicho wakati wa ziara ya baadhi ya Washiriki wa Maonesho ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC juzi.
No comments:
Post a Comment