Habari za Punde

WAZIRI UMMY ATEMBELEA KUKAGUA KLINIKI ZA DHARULA MAONESHO YA WIKI YA VIWANDA KWA NCHI ZA SADC

  WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akimsikiliza Daktari Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya dharula na ajali Dk. Juma Mfinanga, alipokuwa akifafanua jambo kuhusu Chumba maalumu cha dharula kwa ajili ya wageni wanaohudhuria mkutano mkuu wa 39 wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC, wakati alipotembelea maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha.
 Waziri Ummy akipita katika Mabanda kuelekea kukagua Kliniki za Dharula za Jeshi.
 WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akimsikiliza Daktari Bingwa wa Hospitali ya Jeshi (TPDF) Meja Andrew Israel, wakati alipotembelea Banda la Kliniki ya dharula ya Jeshi la Wananchi katika maonesho ya Nne ya Wiki ya Viwanda katika Viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam, yaliyoshirikisha jumla ya nchi 16 za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC . Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.