Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo kuhusu Shirika hilo kusitisha huduma za usafiri wa Treni za abiria na mizigo kwa njia ya Reli ya kati kutokana na njia kuharibiwa na maji ya mvua zinazoendelea kunyesha nchini. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika hilo, Focus Sahani. (Picha na Muhidin Sufiani).
SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limeanza ukarabati wa miundombinu ambayo imeathiriwa na mvua ambazo zinaendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo nchini.
Maeneo hayo ambayo yaliyoathirika ni Kilosa (Morogoro), Gulwe (Mpwapwa), Igandu, Zuzu na Makutupora (Singida).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TRC, Masanja Kadogosa, amesema kuwa mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini zimesababisha kufurika kwa mito mikubwa na kuleta uharibifu mkubwa katika njia ya reli katika baadhi ya maeneo.
Alisema takribani maeneo 26 yameathirika kati ya hayo 10 yapo katika hali mbaya ambapo tuta la relin na baadhi ya makalavati yamezolewa na maji.
“Hali hii imepelekea TRC kuomba radhi kwa wadau wa sekta ya miundominu ya reli kusimamisha huduma za uchukuzi wa abiria na mizigo hasa kati ya Mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma mpaka hapo hali itakapotengemaa na tutawajulisha wadau wa sekta ya miundombinu ya reili, ikizingatiwa kuwa bado mvua zinaendelea kunyesha”alisema
Alisema kutokana na hali hiyo ya uharibifu wahandisi wa TRC wako katika maeneo mbalimbali yaliyoharibika kufanya tathmini halisi ya gharama za miundombinu ya reli iliyoathirika.
“Matengenezo ya muda mfupi yanaendelea katika maeneo ambayo maji yanayopungua ili kurejesha huduma za usafiri wa treni za abiria na miozigo ambapo hadi sasa maeneo ya kati ya Dodoma na Makutupora yamerekebishwa”alisema
Pia alisema katika njia za reli ambazo zimepata uharibifu ambapo maji yamechukua tuta lote ambapo wameamua kusogeza reli kuelekea sehemu za mlimani zaidi au pembezoni.
Na njia ambazo TRC wamepanga kuhamisha miundombinu yao ni kilomita 6 kutoka Kilosa na kilomita 365 katika njia hiyo hiyo ya kilosa.
Alisema kuna sehemu maji yamezunguka reli hapo hatuna namna tunasubiri maji ya shuke ili kuona ni namna gani tunaanza ukarabati.
Mvua zinazonyesha manyara, Singida, Iringa yale maji ambayo yamekuwa yakitiririka ndiyo yanayosababisha athari hizo.
Aliongeza katika mikoa ya Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro, Dar Kwenda Tanga na Kilimanjaro, Mpanda kwenda Taboran Shinyanga, na Mwanza zinaendelea kufanya kazi kama kawaida.
KUHUSU ATHARA
Kadogosa alisema katika suala la uendeshaji wa treni ni kati ya milioni 100 hadi 150 kwa siku hivyo inavyokuja suala la kusimamisha safari ni fedha hizo ambazo zinakuwa zimepotea
Pia alisema katikia suala la kurudishia njia gharama pia ni kubwa kutokana na mzunguko kuwa mkubwa.
“Tukizungumzia hasara ni kubwa sana kutokana na kusimamisha shughuli za usafirishaji kwa siku kadhaa na suala la matengenezo lakini pia hata katika upande wa abiri watapata usumbufu na wengine awatarudi tena,
“Kwahiyo tupo tunafanya tathimini ya kuona ni kiasi gani tutatumia katika suala zima la ukarabati ili kujua gharama kwa ujumla na tutatoa taarifa”aliseama
Aliongeza serikali imekuwa ikichukua tahadhari mbalimbali juu ya kushugulikia tatizo hili lisizidi kujitokeza japo changamoto inakuwa kwa watua ambao wanafanya shughuli za kilimo kuwa kubwa na kufanya mchanga kuzolewa mwingi
KUHUSU ABIRIA WALIOKUWA WANASAFIRI
Alisema katika watu ambao walikuwa wanasafiri kuelekea katika sehemu ambazo usafiri umesimamishwa wapo ambao walifaurishwa kwenda kwa basin a wengine kurudishiwa nauli zao.
“Kunawatu ambao tumeshawasafirisha kwa mabasi na kwa waliokata tiketi tutawarudishia hela zao”alisema
No comments:
Post a Comment