Habari za Punde

BONGE LA MPANGO LA NMB LATOA ZAWADI YA PESA TASLIMU, PIKIPIKI NA GARI

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Donatus Richard (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuchezesha Droo ya mchezo wa kubahatisha wa Bonge la Mpango kwa wateja wa benki hiyo wanaoweka na kuwekewa  pesa katika akaunti zao. Droo hiyo ilichezeshwa katika Tawi la NMB Mbagala Zakiem jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Mkaguzi wa michezo ya kubahatisha, Joram Mtafya (kulia) ni Afisa Huduma kwa Wateja Benki ya NMB Makao Makuu, Neema Deus.
Afisa Huduma kwa Wateja Benki ya NMB Makao Makuu, Neema Deus, akimpigia simu mmoja kati ya washindi wa droo ya  mchezo wa kubahatisha wa Bonge la Mpango kwa wateja wa benki hiyo wanaoweka na kuwekewa  pesa katika akaunti zao wakati wa kuchezesha droo hiyo iliyochezeshwa katika Tawi la NMB Mbagala Zakiem, jijini Dar es Salaam, leo. Katikati ni Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Donatus Richard (kushoto) ni Mkaguzi wa michezo ya kubahatisha, Joram Mtafya.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Donatus Richard, akizungumza na kuonesha moja kati ya magari yanayoshindaniwa katika Droo ya mchezo wa kubahatisha wa Bonge la Mpango, wakati wa kuchezesha droo hiyo iliyochezeshwa katika Tawi la NMB Mbagala Zakiem jijini Dar es Salaam.
Gari likijaribiwa kufunguliwa milango
Sehemu ya magari yanayoshindaniwa yakiwa nje ya Benki ya NMB Tawi la Mbagala Zakiem.
Weka pesa sasa katika Akaunti yako ya NMB ili uweze kuingia katika droo ya kushindania zawadi mbalimbali zikiwemo pesa taslimu, pikipiki, na magari.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.