Habari za Punde

WENYE VITI SERIKALI ZA MITAA, MAOFISA WANOLEWA NA WLAC KUHUSU HAKI ZA WAAJILI NA WAAJILIWA

Mratibu wa mradi wa mafunzo ya Wafanyakazi kwa waajili na waajiliwa, kutoka Kituo cha msaada kwa Wanawake na watoto WLAC, Wakili Abia Richard, akifafanua jambo wakati akifungua rasmi mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mbezi mwisho jijini Dar es Salaam, leo. 
****************************************
Akizungumza katika mafunzo hayo kwa wafanyakazi wa Serikali ya Mtaa Kata ya Mbezi, Abia alisema kuwa Kituo cha WLAC kimeamua kuendesha mafunzo hayo ili Viongozi wa Serikali ya Mtaa waweze kujua haki zao na wajibu wao kwa jamii ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Taasisi hiyo kutoa mafunzo ya aina hiyo ili kuweza kuwafikia walengwa waweze kujua haki zao.
Aidha alisema kuwa kumekuwa na malalamiko na kesi nyingi kutoka kwa Jamii zinazoanzia Ofisi za serikali ya Mtaa na Kata ambapo baada ya kupata Elimu hiyo watakuwa Mabalozi wazuri wa kuwaelimisha wenzao na Wananchi kwa ujumla.
''Katika Jamii pia kuna wafanyakazi wa ndani ambaye pia ana haki zake za kuajiliwa kama mfanyakazi, lakini pia Waajili wamekuwa hawajui haki zao na za wafanyakazi wao wa ndani kwa kutojua ambapo wamekuwa hawawapatii mishaara kwa wakati na haki zao nyingine, hivyo kwa mafunzo haya naamini wengin wetu tutakuwa mabalozi wazuri kwa kutoa elimu kwa wengine na wafanyakazi wa ndani pia ili waweze kujua haki zao kama wafanyakazi. amesema Abia
Mafunzo haya yatakua ni chachu ya mabadiliko kwa wananchi wanaoishi katika Kata zao kuweza kumtambua mfanyakazi wa ndani, ambaye pia anawajibu wake kama muajiliwa na wafanyakazi wa katika Mahoteli na mabaa nao wakapewa haki kama ambavyo wafanyakazi wengine wanapewa haki na kujua wajibu wao, ikiwa ni pamoja na kuwalipa mishahara yao kwa wakati.
Alisema kuwa Taasisi hiyo baada ya kufanya utafiti waligundua kuwa kumekuwa na unyanysaji na ukatili mwingi unaoendelea katika Mabaa ambapo hata wafanyakazi wengine wamekuwa hawapati kazi bila kutembea aidha na Meneja ama Mwenye Baa na wengine kushikwa maumbile yao bila ridhaa zao wakiwa katika maeneo yao ya kazi na mambo kadha wa kadha yanayokiukwa na waajili wao.
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Msakuzi, Nicholaus Ntinika, alisema kuwa mafunzo hayo yamewafungua akili na kuongeza kuwa watakwenda kuwa mabalozi wazuri katika mitaa yao na kutoa mafunzo waliyopatiwa ili kufikisha ujumbe kwa waajili na waajiwa katika jamii zinazowanguka.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo, Wenyeviti wa Serikali za Mtaa, Maofisa Ustawi wa Jamii, Maofisa Kilimo, Maofisa Mifugo na Maofisa Uvuvi, wakifuatilia mafunzo hayo leo.
Mwendesha mafunzo hayo kutoka Kituo cha msaada wa sheria kwa Wanawake na Watoto, WLAC, Zaituni James, akitoa mafunzo kwa washiriki.
Zaituni akigawa Vipeperushi kwa washiriki wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wakipitia vipeperushi kwa umakini baada ya kukabidhiwa wakati wa mafunzo hayo.
Mshiriki akichangia kujadili moja ya hoja zilizotolewa katika mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.....Mafunzo yakiendelea...

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.