Habari za Punde

YANGA YAIGOMEA SIMBA KWA MKAPA 'KILA MTU AJIBEBE'

Mshambuliaji wa Yanga Yacouba Sogne (kulia) akimtoka kiungo wa Simba, Erasto Nyoni wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliomalizika hivi punde katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga imeshinda bao 1-0 bao lililofungwa na Zawadi Mauya katika dakika ya 11 ya kipindi cha kwanza bao lililodumu hadi kumalizika kwa mchezo huo. Picha na Muhidin SufianiKiungo wa Yanga, Feysal Salum 'Fey Toto' akiwa katikati ya msitu wa mabeki wa Simba....Zawadi Mauya (kulia) akipiga shuti lililozaa bao la kuongoza na la ushindi kwa timu yake.....Kiungo mkabaji wa Yanga, Mukoko Tonombe akishangilia ushindi.....Tuisila Kisinda akimtoka beki wa Simba Taddeo Lwanga, wakati wa mchezo huo......Beki wa Simba, Mohamed Hussein (kushoto) akijaribu kuondosha mpira huku akizongwa na Said Ntibazonkiza, wakati wa mchezo huo.

KWA MATUKIO KAMILI YA PICHA NA VIDEO ZA MTANANGE HUU KAA NASI HAPO BAADAYE 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.