Habari za Punde

UJENZI WA RELI YA KISASA SGR MAKUTUPORA-TABORA

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) akifunua kitambaa kuzindua rasmi Jiwe la msingi la Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Makutupora-Tabora wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika eneo la Cheo mkoani Tabora. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Batilda Buriani na baadhi ya viongozi. (Picha na Muhidin Sufiani)
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akifurahia baada ya kuzindua rasmi Jiwe la msingi la Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Makutupora-Tabora wakati wa hafla ya uzinduzi huo.Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi uwekaji wa Jiwe la msingi la Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Makutupora-Tabora wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika eneo la Cheo mkoani Tabora jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania TRC, Masanja Kadogosa (wa pili kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Batilda Buriani na baadhi ya viongozi.
Waziri Makame Mbarawa, akisalimiana na baadhi ya viongozi baada ya kuwasili katika viwanja vya Cheo mkoani Tabora alipofika kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya kisasa SGR.Waziri Makame Mbarawa, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa NSSF Lulu Mengele baada ya kuwasili katika viwanja vya Cheo mkoani Tabora alipofika kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya kisasa SGR.Waziri Makame Mbarawa, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Benki ya NMB alipotembelea katika banda lao baada ya kuwasili katika viwanja vya Cheo mkoani Tabora alipofika kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya kisasa SGR.
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Said Chege (Chege Chigunda) akiimba na kuwachezesha baadhi ya viongozi katika hafla hiyo.
Msanii wa muziki wa Singeli, Balobalo akitoa burudani jukwaani wakati wa hafla hiyo.
kurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania TRC, Masanja Kadogosa, akipiga ngoma sambamba na wasanii wa kikundi cha ngoma ya asili cha Mawege cha mkoani Tabora wakati kilipokuwa kikitoa burudani katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR) iliyofanyika katika eneo la Cheo mkoani Tabora 
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB wakishiriki katika hafla hiyo.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Said Chege (Chege Chigunda) akiimba mbele ya wananchi wakati akitoa burudani katika hafla ya uzinduzi wa uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Reli ya kisasa SGR iliyofanyika katika eneo la Cheo mkoani Tabora.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.