Habari za Punde

KATIBU MKUU UCHUKUZI AWATAKA WATUMISHI KUWA WABUNIFU

Katibu Mkuu-Uchukuzi, Gabriel Migire akitoa maelekezo kwa Meneja wa Huduma za Meli Mkoa wa Kigoma, Alen Butembero (kushoto) wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea mradi wa Ukarabati wa Meli ya MT. Sangara mwishoni mwa wiki.
Mwonekano wa hatua iliyofikiwa ya ukarabati wa Meli ya MT. Sangara  katika Bandari ya Kigoma. Ukarabati wa Meli hiyo unafanywa na Kampuni ya KTMI ya nchini Korea ya Kusini ambapo ukarabati wake unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwaka huu na itakuwa na uwezo wa kubeba mafuta lita takribani 410,000 .
Katibu Mkuu sekta ya Uchukuzi Gabriel Migire (kushoto) akitoa maelekezo kwa Meneja Miradi wa Mamalaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bakari Mlima, wakati alipotembelea mradi wa Bandari Kavu ya Katosho, mjini Kigoma mwishoni mwa wiki.
************************************** 
Serikali imetoa wito kwa watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Sekta ya Uchukuzi kuongeza ufanisi na ubunifu ili kuongeza tija kazini na kukuza mapato ya Taasisi hizo na Taifa kwa ujumla. 
Akizungumza mjini Kigoma Katibu Mkuu (Sekta ya Uchukuzi), Gabrieli Migire, amesema ukuaji wa biashara mkoani humo unategemea sana miundombinu ya usafiri na uchukuzi hususani bandari na reli na kutoa wito kwa watumishi kuzidisha kasi ya utendaji ili kufikia lengo hilo. 
“Mkoa huu una bandari una reli ongezeni kasi ya utendaji kwani kukua kwa pato kwa taasisi za uchukuzi kwanza kutafanya taasisi kununua mitanbo zaidi lakini kupokea na kusafirisha mwingi zaidi na kuonegza pato la taasisi, mkoa na Taifa kwa ujumla", amesema Katibu Mkuu Migire. 
Aidha, amemtaka Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), Eric Hamiss, kuhakikisha miradi ya bandari inayotekelezwa mkoani humo inakamilika kwa wakati na viwango huku akisisitiza uadilifu katika utekelezaji huo ikiwemo bandari za Ujiji, Kibirizi, Bandari Kavu ya Katosho. 
Kwa upande wake Meneja wa Bandari ya Kigoma, Manga Gassaya, amesema kwa sasa Bandari hiyo inauwezo wa kuhudumia tani milioni tatu kwa mwaka na mzigo unaosafirishwa kwa sasa unapelekwa Burundi, DRC -Congo na Rwanda. 
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Migire amekagua mradi wa ukarabati wa meli ya MT Sangara na kumtaka  Meneja wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) wa mkoa wa huo, kuhakikisha kasi ya ukarabati huo inaongezeka ili kukamilisha mradi huo na kuruhusu usafirishaji wa mafuta kutoka Kigoma na nchi zinazozunguka Mkoa huo. 
Naye, Meneja wa kampuni ya MSCL wa mkoa huo, Allen Butembero, amesema ukarabati wa meli ya MT. Sangara unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2022 na itakapokamilika  itakuwa na uwezo wa kubeba mafuta lita 410,000. 
Katibu Mkuu Migire yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya Sekta ya Uchukuzi. 
(Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi)

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.