MABEHEWA MAPYA 21 KWENDA KIGOMA Kadogosa amesema mabehewa mapya yaliyokuwa yakifanyiwa majaribio kwa mujibu wa sheria baada ya kupitishwa na Mamlaka ya Usafiri Ardhini (LATRA) na kuona yanakidhi mahitaji ya kusafirisha abiria.
“ Hatimaye leo tumeanza safari rasmi kwa kutumia mabehewa mapya 21 ya Meter Gauge (MGR) kwenda Kigoma na treni itakaporejea Dar es Salaam, itaanza safari ya kwenda Kilimanjaro ambapo mabehewa hayo yatasaidia kupunguza msongamano wa abiria kugombania upatikanaji wa tiketi,” amesema.
Mabehewa hayo yalinunuliwa na serikali kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kutoa huduma ya usafiri wa reli nchini.
Aidha Kadogosa amesema safari rasmi zimeanza baada ya majaribio ya awali umbali wa kilometa 400 kutoka Dar es Salaam –Morogoro ambapo LATRA imeridhia mabehewa hayo kuanza kazi rasmi.
Mabehewa mapya ya abiria ni 20 ambayo yamebeba jumla ya abiria 1500 wanaotoka Dar es Salaam kwenda Kigoma huku behewa moja likitengwa kwa ajili ya huduma za mgahawa.
“Kufuatia ununuzi wa mabehewa hayo, Shirika hilo limeongeza idadi ya mabehewa ya treni ya Deluxe kwenda mikoa ya Kaskazini kutoka mabehewa sita hadi 16 na njia ya reli ya kati kutoka mabehewa 4 hadi 20,” alifafanua.
Alisema TRC itaongeza idadi ya mabehewa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu watakaojitokeza kutumia usafiri huo.
Akizungumza na Blog hii mmoja kati ya abiria waliosafiri na treni hiyo, aliyejitambulisha kwa jina la Sheha Ibrahim, amesema kuwa mabehewa hayo yako vizuri na yakiendelea hivyo yatavutia watu wengi kutumia usafiri wa treni na kuachana na mabasi.
‘’Nauli ya usafiri huo haijaongezwa kwani wanatumia za zamani za treni ya deluxe ambayo kwa daraja la kulala ilikuwa sh. 65,000 kutoka Dar es Salaam- Kigoma.
‘’ Ni ukombozi kwetu Watanzania kupata mabehewa kama haya kwa sababu yaliyokuwepo hayana hali nzuri hivyo itatusaidia sisi kuachana na mabasi,” amesema.
Desemba 6, mwaka huu, jumla ya mabehewa mapya 22 yalikamilisha taratibu za kufanya majaribio kutoka Dare s Salaam - Morogoro na kurudi na LATRA kuridhia kuanza kubeba abiria nchini.MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa, akimkabidhi dereva wa Treni, Line clear ili kuanza safari yake ya kutoka Dar es Salaam kuelekea Kigoma wakati wa uzinduzi wa safari hiyo kwa kutumia mabehewa mapya 21 kati ya 22 yaliyowasili hivi karibuni. Treni hiyo imeondoka jana baada ya kufanyiwa majaribio Desemba 6 mwaka huu na kupewa kibali na LATRA. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano TRC, Jamila Mbarouk. (Picha na Muhidin Sufiani)MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa, akipeperusha bendera kuashiria kumruhusu dereva wa Treni,kuanza safari yake ya kutoka Dar es Salaam kuelekea Kigoma wakati wa uzinduzi wa safari hiyo kwa kutumia mabehewa mapya 21 kati ya 22 yaliyowasili hivi karibuni. Treni hiyo imeondoka jana baada ya kufanyiwa majaribio Desemba 6 mwaka huu na kupewa kibali na LATRA. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano TRC, Jamila Mbarouk.BAADHI ya abiria wakipanda Treni ya kuelekea Mkoani Kigoma katika kituo cha Kamata Dar es Salaam, jana ambapo kwa mara ya kwanza abiria hao wamesafiri kwa kutumia mabehewa mapya yaliyowasili hivi karibuni. BAADHI ya abiria wakipanda Treni ya kuelekea Mkoani Kigoma katika kituo cha Kamata Dar es Salaam, jana ambapo kwa mara ya kwanza abiria hao wamesafiri kwa kutumia mabehewa mapya yaliyowasili hivi karibuni.Abiria akipitisha mzigo dirishani akimpa mwenzake ili kumuwekea nafasiAbiria akipitisha mzigo dirishani akimpa mwenzake ili kumuwekea nafasiBaadhi ya abiria wakiwa ndani ya Treni hiyo wakipanga mizigo yaoBaadhi ya abiria wakiwa ndani ya Treni hiyo wakiwa na furaha kwa kupanda mabehewa mapya
No comments:
Post a Comment