Habari za Punde

SAKATA LA FEY TOTO, AZAM VS YANGA MBUZI KAFIA KWA MUUZA SUPU

KUTOKANA na kile kinachoendelea mitandaoni kuhusu sakata la mchezaji Feysal Salu (Fey Toto|) Hatimaye Klabu ya Yanga imeibuka na kutoa tamko rasmi kuhusu mchezaji wao na kuhusu sgeria na kanuni zitakaziomruhusu mchezaji aliye ndani ya mkataba kuanza mazungumzo na Klabu nyingine.

TAMKO la KLABU 
KLABU YA yANGA inapenda kuujulisha umma na Wanachama wa Yanga kuhusiana na taarifa za mchezaji wetu Feisal Salum Abdallah zinazoenea katika mitandao ya kijamii.
Klabu inathibitisha kupokea barua kutoka kwa mchezaji tarehe 23 Disemba 2022 inayoeleza kuvunja Mkataba wake baina yake na Klabu.
Klabu ya  Young Africans Sports Clubimemuandikia na kumjibu Feisal na miongoni mwa majibu ni kama ifuatavyo;
Hakuna misingi ya kikanuni wala kisheria kulingana na mkataba wake ambazo zinampa haki mchezaji kusitisha mkataba wake na Klabu kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba wa sasa
Kanuni na Taratibu za FIFA ziko wazi na zimeelezea taratibu zote juu ya Jambo la aina hii.
Kwamba, Mkataba baina ya mchezaji na Klabu hauwezi kuvunjwa na upande mmoja tu bila kujadiliana na upande wa pili wakati msimu wa ligi ukiwa unaendelea.
Kwamba, kwa mazingira hayo, barua ya mchezaji ina dhana potofu na haina misingi ya kisheria ya kuvunja mkataba baina ya klabu na mchezaji.
Na kwa mantiki hiyo, tumemuagiza Feisal, azingatie matakwa ya mkataba wake kama ilivyoelezwa katika mkataba huo.Klabu pia imemkumbusha Feisal, mkataba wake wa sasa ni halali hadi ifikapo Tarehe 30 Mei 2024.
Pamoja na hayo, tunapenda kuujulisha umma kuwa, kwa kuthamini kiwango na mchango wa Faisal kwa klabu yetu, tayari tulishaanza mazunguzo baina ya klabu ya Yanga na wawakilishi wa Feisal wakiongozwa na mama mzazi wa mchezaji ili kuboresha maslahi yake na kuongeza muda wa mkataba wake wa sasa ambao unaishia Mei 2024.
Hata hivo, Klabu haijapokea majibu mbadala wa mapendekezo ya maboresho haya kutoka upande wa Feisal na wawakilishi wake na badala yake tumepokea barua inayoelezea kuvunja mkataba kutoka upande wa Feisal ambayo ni Kinyume na makubaliano ya mkataba wake wa sasa.
Klabu tayari imesharejesha fedha kiasi cha TZS 112,000,000 (Millioni Mia Moja na Kumi na mbili) ambazo Feisal aliziweka katika Akaunti za Klabu.
Tunapenda kueleza kuwa, kuna taratibu na kanuni za Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) .

KILE ALICHOKIANDIKA FEYSAL SALUM TOTO KATIKA UKURASA WAKE WA FACEBOOK KUWAAGA MASHABIKI WA YANGA.
 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.