Mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga leo wanaanza kampeni ya kuwania taji la Mapinduzi watakaposhuka uwanja wa Amaan kupepetana na KMKM mchezo utakaopigwa saa 2:15 usiku.
Ni mchezo muhimu kwa Yanga kupata ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.
Singida Big Stars walishinda mabao 2-0 walipokutana na KMKM hivyo Yanga inahitaji ushindi pia kabla ya mchezo dhidi ya Singida Big Stars.
Jana watani zao Simba waliondoshwa mapema kwenye michuano hiyo baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Mlandege Fc .
Katika mchezo huo Yanga inatarajiwa kuwatumia nyota wake Lazarus Kambole, Yacouba Sogne ma Mudathir Yahya ambaye alitua Visiwani Zanzibar mapema jana baada ya kukamilisha usajili wake na Yanga
Yacouba na Kambole watakuwa kivutio kwa Wananchi kwani kila mmoja anatamani kuwaona uwanjani hasa Yacouba ambaye anakubalika kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuucheza mpira.
Kabla Yacouba hajapata majeraha alikuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi cha Yanga akifunga mabao muhimu sana na uwezo wake wa kuamua mechi ulikuwa mkubwa
Wananchi wanatamani kumuona baada ya kumkosa uwanjani kwa muda mrefu akisumbuliwa na majeraha ya goti ambayo hata hivyo alipona muda sasa.
No comments:
Post a Comment