Habari za Punde

KASEBA ACHAKAZWA NA CHEKA, ATEPETA RAUNDI YA TISA

Kaka mie si Kick Boxer tu hata ngumi naweza na hiyo ni salam tu...........Hii ilikuwa ni raundi ya tatu ya mchezo wa raundi 12, Fransic Cheka, akiwa chini baada ya kusukumiwa konde ziti na mpinzani wake, Japhet Kaseba, wakati wa mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam jana. Picha na (SPM)
We jiti wajua tu mie nasoma mchezo wako tu, ntakuanzishia baadaye kidooogo...........Kaseba (kulia) akijitahidi kusukuma makonde mazito kabla jamaa hajachukia, baadaye mambo yaliharibika, kwani Kaseba alikalishwa katika raundi ya tisa ya mchezo na mchezo huo ukavunjika kutokana na vurugu za mashabiki, walioingia ulingoni. Picha na (SPM)
Ndiyo naanza kazi sasa ohoooooooo.................Cheka naye alianza kazi ya kumchakaza Kaseba katika raundi ya tano kwa makonde mazito, ambayo yalimchanganya vibaya na kupoteza muelekeo. Picha na (SPM)

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.