Twende mdogo wetu ushawamwaga sasa hivi we ndo bosi....hawachelewi kuiba hata hii naniliu...
Mshindi wa shindano la Bongo Star Search, Pascal Kassian, akiwa chini ya uangalizi wakati akishuka jukwaani baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya Sh. milioni 25 alipotanganzwa mshindi kwa kuwabwaga washindani wenzake wanne. Picha Zote na (SPM)
Wacha niwapagawishe masela wangu ili wanipigie kura, "pigeni kura pigeni kura masela nikamate mahela".......
Mshiriki wa shindano hilo, Beatrice William akitupa karata yake ya mwisho.
Kama mnapenda poa kama hampendi nipotezeeni tuuuuu...., ila hiki kivazi na wimbo huu sijui..........
Beatrice akipagawisha na kete yake ya kwanza kwa kuimba wimbo wa dini wa Rose Mhando.
Mtanikubali tu si mlizani ninamiondoko ya pasta tuuu, me ka Ronaldo napiga miguu yote....
Pascal Kassian akitupa kete yake ya pili jukwaani.
Jamani nimekubali matokeo lakini poa tu, huyu jamaa ni mkali apewe haki yake me niko fea...
Mshiriki, Jackson George, akisalimiana na mashabiki baada ya kumalizika shindano hilo na kuitangazwa Kassian kuwa mshindi.
Mashabiki mbona hamshangilii kama mnavyomshangilia Kassian????????????
Naye Kelvin Mbati alifanya vyema katika kuonyesha angalau ushindani, lakini bahati kwa mashabiki haikuwa yake, hapa alikuwa akiimba kibao cha Msanii Marlow.
Jamani huu ndo wimbo wetu tuliotunga na kuimba kwa pamoja wakati tukiwa kambini.
Wasanii watano bora wa shindano la BSS, wakiimba kwa pamoja jukwaani wimbo walioshirikiana kutunga kwa pamoja.
Madam si unaona mabadiliko? Kassian anafunika na mashabiki hawatakubali, Hapana bwaaaana tusibadilishe matokeo tumpe tu yule naniliu.........
Majaji Madam Ritha (kushoto) na Master J, wakishauliana jambo wakati shindano hilo likiendelea jukwaani.
Duh! hapa leo ipo kazi sijui itakuwaje.....Madam anataka kumng'ang'ania naniliu......
Master J, akitafakali.....
Nimepokea meseji sasa hivi kutoka Jidah, naniliu anasema we mkali huna mpinzani eeeh....
Madam Ritha akitoa pont zake kwa mshiriki, baada ya kumaliza kuimba.
Ehee nilisahau na Salama amenitumia meseji kasema unatisha anakutakia ushindi......
Hivi vyote vilikuwa ni vituko vya Madam Ritha ukumbini wakati wa shindano hilo.
Hah!, jamani nashindwa hata kuongea huyu naniliu anaweza jamani, nasimama itakavyokuwa na iwe...
Madam Ritha katika pozi la kumsifia mshiriki, lililomfanya kuwa kimya kwa sekunde kadhaa kabla ya kuanza kusema na kuwashawishi mashabiki kuimba"simama simama simama".
Aaaa jamani ntasimama basi nyamazeniiiii wote wanaweza.........
Madam Ritha akiandaa pozi la kusimama.
Duh! wamenikalia kooni ngoja nisimame........
Baada ya pozi hili ilimbidi asimame na kunyooha mikono na kushangiliwa na mashabiki waliojazana ukubini humo.
Si mmeridhika jamani nimesimama kwa wote lakini naniliu ni zaidi jamani......
Madam Ritha akiwa haamini kinachotokea ukumbini kwa mashabiki kumtaka asimame baada ya Kassian kumaliza kuimba.
Lakini haka kajamaa kanaweza bwana wacha tukape tu, mashabiki watatuua humu ukumbini....
Madam Ritha (kulia) akimsisitiza jambo Jaji mwenzake J. Kitime, wakati sindano hilo likiendelea.
Aaah! uzalendo umenishinda jamani wacha nishangile tu................
Madam Ritha akishangilia wakati akiwa kwenye eneo lake na kujaji shindano.
Hata sisi uzalendo umetushinda wacha tushangile bwana haka kajamaa kamefunika......
Kitime (kushoto) na Master J (kulia) nao wakishangilia.
Wacha tushangile kwa bidii ole wao majaji wasimpe ushindi naniliu kawafunika mbaya......
mashabiki lukuki wakishangilia wakati kassian akiimba wimbo wake wa mwisho uliowafanya mashabiki hao kujaa jukwaani na kumtunza mahela kibaaaaaao.
Hata kama Kigoma tumeshindwa lakini Mwanza si mbali sana mpeni tu Kassian jamaniiiii 
Mkurugenzi wa Aset Club, Asha Baraka (katikati) akishangilia kwa nguvu zote wakati Kassian akishambulia jukwaa, akiwa pamoja na mashabiki wengine kulia ni muhindi ambaye muda wote alipopanda Kassia hakukaa chini alikuwa akiimba na kucheza.
Duh! Kigoma tutatoka kweli haka kajamaa kanaimba utadhani kameutunga kenyewe muziki huu....
Mbunge wa Kigoma Mashariki Kabwe Zotto (katikati) akiwa na badhi ya mashabiki wenzake wakifuatilia shindano hilo.
Hapa hakuna jua wala mvua ila lolote laweza kutokea msinishangae sana jamani........
Shabiki akiwa amepozi katika siti yake huku akiwa na mwamvuli ambao mara nyingi hupenda kutumiwa na wapiga picha wanapokuwa kazini na hasa mpirani ama watu wakia Beach kwa ajili ya kujizuia na jua, lakini rijamaa limeutinga usiku ukumbini huku rikiwa harina wasiwasi.
Aaai jamani haka kajamaa kanaweza hebu kacheki kanavyocheza na kuimba... 
Shabiki akifuatilia shindano hilo lililokuwa likiendelea jukwaaani.
Ngoja nikapige picha haka kakijana kwani kamenikuna sana, na pia itakuwa ni ushahidi wasipokapa ushindi .................
Shabiki akipiga picha ya kumbukumbu.
No comments:
Post a Comment