Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya simu za mkononi Zain Tanzania, Khaled Muhtadi, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Pamoja Plus, iliyozinduliwa jijini leo. Kushoto ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Kelvin Twisa. Picha na (SPM)
DEREVA MWANAMAMA APAGAWA BAADA YA KUTUMBUKIZA GARI LAKE MTARONI
Dereva wa gari dogo ambaye hakuweza kufahamika jina lake, akiwa ameketi kwenye mtaro akilinda gari lake baada kupata ajali maeneo ya Mtaa wa Olympio Dar es Salaam leo. Haikuweza kufahamika chanzo cha ajali hiyo. Picha na (SPM)
MAMA AANGUA KILIO NJE YA MAHAKAMA KUU, KISA..............
Mama ambaye hakuweza kufahamika jina lake mapema, akiangua kilio nje ya Mahakama Kuu Dar es Salaam leo mchana, huku akizungukwa na watu wakimtaka aeleze kilichomsibu hadi kumpelekea kulia hadharani, bila kuwa na majibu huku akiendelea kulia, jambo lililomfanya askari Magereza kufika eneo hilo na kumsaidia kwa kumuinua chini. Picha na (SPM)
PWEZA, NGISI MTAANI BILA KUFUNIKWA NI SALAMA?.....................
Mfanyabiashara wa Ngisi na Pweza, akisubiri wateja wake katika Kituo cha daladala cha Kivukoni, huku akiwa ameachia biashara yake hiyo bila kufunika jambo ambalo linaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko kwa wateja wake. Picha na (SPM)
No comments:
Post a Comment