Habari za Punde

BUSTA ALIVYOWAPAGAWISHA WABONGO NA FIEST DAR

Huyu pia ni msanii wa miondoko ya kufokafoka ambaye aliibukia kwa michano ya Hipo Hop, Witness, akimshangilia Busta alipokuwa akipagawisha jukwaani. Picha Zote na (SPM)

Fid Q, akishambulia jukwaa.

Adam Mchomvu (kushoto) na naniliu nao pia wakishambulia jukwaa eti nao wanananiliuuuuuuuu

Queen Sendiga, mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti ambao walikuwa ni miongoni mwa wadhamini wa Tamasha hilo kubwa na Fiesta (watatu kushoto) akiwa na wenzake wakifuatilia tamasha hilo.

Washkaji nao hawakuwa nyuma katika kupata picha za kumbukumbu Jukwaani ni J. Kusaga akipozi na Busta.

Mashabiki wakisongamana kuwa nafasi za mbele ili kuweza kumuona vyema Busta, wakati wa Tamasha hilo.

Busta na mchizi wake wakishambulia jukwaa.



Wasanii nao hawakuwa nyuma kujifunza jambo kwa mchizi Busta.

Busta akiendelea kushambulia jukwaa kwa staili za kiaina.

Ni mapozi tu ndo yanabadilika.

Mabaunsa nao walifanya kazi ya ziada kuonyesha kuwa mshiko waliolipwa kwa kazi hiyo ilikuwa ni halali, hapa wakijitahidi kuwazuia mashabiki waliokuwa wakitaka kuvuka uzio ili kufika mbele kabisa ya jukwaa.

Bahati Singh wa Serengeti Bia (watatu kushoto) akiwa na washkaji wakifuatilia tamasha hilo.

Hawa ni miongoni tu kati ya mashabiki lukuki waliofurika kwenye Tamasha hilo la Fiesta linalofanyika kila mwaka.

Busta na mchizi wake wakipagawisha.

Huyu si mnenguaji la hasha bali ni mchizi Chidi Benz, akipagawa na miondoko ya Busta mara bada ya kushuka jukwaani.

Hawa nao ni baadhi ya watangazaji wa Clouds Fm, wakijimiksi.

Busta jukwaani.

Chid Benz, akiendelea kupagawa.



Na hawa ni baadhi ya wasanii wa miondoko ya Bongo Flava, Dully Sykes (kushoto) na Mr. Blue, wakifuatilia Tamasha hilo.



Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Serengeti, Teddy Mapunda (kushoto) akiwa na washkaji wakifuatilia Tamasha hilo la One Love.

Starehe gharama bwana..., haka kabinti eti kalijaribu kupima ubavu na minjemba yenye usongo wa kumuona Busta, kakawahi nafasi ya mbele kabisa matokeo yake kaliminywa nusu ya kudedi, kaliokolewa na mabaunsa hapa kakipewa huduma ya kwanza, hakarudii tena 'kudanganyika'...


Eti nae huyu kama naniliuuuuuu...............Sijui anajiona kama naniliu jukwaani?????????????

Huyu si chapombe bali kajichetua tu na mapigo yake kama naniliu, hapa kinywaji cha mnyama Serengeti kimeshafanya kazi.

Hawa watangazaji wa Clouds Fm, sijui walikuwa wakicheza ama wakiimba kwani walionekana muda wote wakiwa bize kinomaaaaaa.

Hapa sasa wamejimiksi na washkaji fani yao wameweka kando kabisaaaaaa.

Hii ni alama ya Tamasha hilo 'ONE LOVE'....

Huyu ni mchizi Chid Benzi akikubali yaishe akimpigia saruti mshkaji Busta. WE MKALIIIIIIIIII


































No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.