Habari za Punde

MAANDALIZI YA UJIO WA KOMBE LA DUNIA NCHINI

Hili ni moja kati ya majukwaa yaliyojengwa kwenye Uwanja wa Taifa, litakalotumika wakati wa kuonyesha Kombe hilo linalotarajia kuwasili nchi kesho na kupokelewa na mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete.
Eti na huyu msanii wa ze nini vileeee, naniliu Mkandamizaji, akipiga picha ya kumbukumbu baada ya kuingia ndani ya Uwanja wa Taifa, wakati wa maandalizi ya uwanja huo utakao tumika kwa maonyesho ya Kombe hilo.


Hili nalo ni jukwa jingine lililojengwa nje ya Uwanja huo.

Jinsi Uwanja huo unavyoonekana baada ya kuweka alama zitakazotumika kupitia wakati wa kuangalian na kupiga picha na Kombe hilo.

Eti na warembo nao hawako nyuma katika kusaka mshiko, hapa wakiwa nje ya uwanja huo wakisubiri kupewa maelekezo ya jinsi watakavyofanya kazi siku hiyo kutoa huduma mbalimbali, nadhani hawa woooote unawafahamu mwanasufianimafoto huwezi kudanganyika ama nikutajie????.

Hawa hawasaki mshiko ila inaitwa saka nyoka, ni waandishi wa habari, Somoe Ng'itu wa la Nipashe (kulia) na Zena Chande wa Gazeti la Habari Leo, nao wakiwa eneo la tukio kupata kinachojili ili kuwafikishia wasomaji wa magazeti yao kuhusu ujio wa Kombe hilo ikiwa ni pamoja na ratiba kamili.

Hii ni sehemu ya nje ya Uwanja huo ilivyopambwa ikiwa imesheheni miamvuli ya washkaji wa Cocacola, ambao ndiyo wadhamini wakuu wa ujio wa Kome hilo.






No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.