Habari za Punde

MATUKIO YA WIKI JIJINI DARA KATIKA PICHA

MATUKIO YA SIMBA, YANGA KATIKA PICHA

Huyu katika picha tunamjua pichani si Nd....huyu eti karipa hiri rijamaa ritkitumie kuingia.....

Askari polisi wakionyesha Kitambulisho cha mmoja wa Viongozi wa timu ya Simba, kilichokamatwa akiwanacho shabiki wa timu hiyo akijaribu kukitumia ili kuingia ndani ya Uwanja wa Taifa, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania bara kati ya Yanga na Simba, mwishini mwa wiki iliyopita.

Ushindi mtamu jamani eeh......SebeneeeeeeeeeMwenyekiti wa Simba, Hassan Dalali (wapili kulia), Katibu wa timu hiyo, Mwina Kaduguda (kulia) na mchezaji, Mohamed Banka (kushoto), wakicheza mdundiko kwa furaha kushangilia ushindi wa timu yao mara baada ya mchezo baina yao na Yanga kumalizika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam juzi. Simba ilishinda 1-0. Picha Zote na (SPM)

Mliyataka wenyewe sasa mmeyapata mwalia niniiiiiiiiiiii, Simba kidume ...........Mashabiki wa Simba, wakishangili ushindi wa timu yao mara baada ya mchezo kumalizika.

hata muwe sita kwa pamoja hapa hampiti, unapiga kelele za nini cheza soka weweeeee......Beki wa Yanga, Mohamed Bakari (chini) akichuana kuwania mpira na washambuliaji wa Simba, Mussa Hassan Mgosi na Hillary Echessa (kulia) wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi. Simba ilishinda 1-0.

Dogo huuwezi huu moto utabaki kunishika kwa mikono tuu, si unacheki vitu hivi?.......
Mshambuliaji wa Yanga, Moses Odhiambo (kulia), akiruka kumiliki mpira mbele ya Beki wa Simba, Juma Jabu.

Nasiki wewe ndo mwiba hapa umekutana na msumari mafuruku yako huko huko...kakaaaa.....Beki wa Yanga, Amir Maftah, akimiliki mpira mbele ya mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (kushoto), Kuliani Kigi Makassy, akisubiri kutoa msaada.

Hapa hupiti wewe hata upige kerere vipi ...............Beki wa Simba, Kelvin Yondani (kushoto) akichuana kuwania mpira na mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete, wakati wa mchezo huo.


FM ACADEMIA WATAMBULISHA VUTA NIKUVUTE JIJINI DAR
Waimbaji na wanenguaji wa Bendi ya Fm Academia, wakishambulia jukwaa wakati wa onyesho lao la utambulisho wa nyimbo zao mpya zitakazokuwa kwenye albam yao ijayo itakayojulikana kwa jina la Vuta Nikuvute. Picha Zote na (APM)


Wanguaji wa kike wa Fm Academia wakishambulia Jukwaa kwa pamoja, katika Vuta Nikuvute.

Mwimbaji wa bendi hiyo, Alfabet Kalbeza, akiimba wimbo wake mpya alioutunga wakati akiwa safarini Abidjan.

Kiongozi wa Bendi hiyo, Nyosh El-Saadat (wapili kulia) akishambulia jukwaa na waimbaji wenzake wakati wa onyesho hilo.


WASHIRIKI WA BSS WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

Hongera sana umeweza kuonyesha kipaji chako........Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Production, Ritta Paulsen (kulia) akimkabidhi hundi ya Sh. milioni 25, mshindi wa shindano la Bongo Star Search, Pascal Kassian, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Katikati ni Ofisa Mwandamizi Mkuuwa Kitengo cha Utafiti BASATA, Vicky Temu.

Eh bwana eeeh siamini zote zangu hizi????????????duh.............Huyu ni mshindi wa tatu katika shindano hilo, Kelvin Mbati, akiwa haamini macho yake kwa kile alichokuwa akikabidhiwa na Mkurugenzi wa Benchmark Production, Ritta, Paulsen, wakati wa hafla hiyo.

Sijui hizi pesa nitazifanyia nini ili nisijeonekana nimefulia, ila ningepata za naniliu ..........wangeni...Kelvin Mbati katika wimbi la mawazo juu ya mshiko aliokabidhiwa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.