Habari za Punde

RAIS JK AZINDUA JENGO LA KITENGO CHA MATIBABU YA DHARULA DAR

Hivi ndivyo jengo la Matibabu linavyoonekana, jengo hili ambalo awali lilikuwa ni jengo la mapokezi ya Hospitali ya Muhimbili, linavyoonekana baada ya kukamilika.

One Two Three cut..........
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Abolt Fund Tanzania, Christ Wiston (kushoto) na Mwakilishi wa Balozi wa Marekani nchini, Larry Andre (kushoto kwa Rais) na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Davis Mwakyusa (kulia) wakikata utepe kuzindua jengo la Kitengo cha matibabu ya Dharula, lililopo Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, uzinduzi huo ulifanyika leo. Picha na (SPM)

Rais Jakaya Kikwete, Eddy Bergaman (kulia) Anne Klamar (katikati), John Spencer (wapili kushoto) na Stan Bergman, wakikata utepe kwa pamoja kuzindua jengo la Shule ya Meno ya Chuo Kikuu cha Muhimbili Dar es Salaa leo.

Kwakweli mmejitahidi kuboresha.....
Rais Jakaya Kikwete, (kulia) na baadhi ya Viongozi wa Serikali wakitoka kukagua jengo la Shule ya Meno ya Chuo Kikuu cha Muhimbili, mara baada ya kuzindua jengo hilo leo.

Mkuu wa Shule ya Meno ya Chuo Kikuu cha Muhimbili, Dk. Elifuraha Mughamba (kushoto) akitoa maelezo ya Jengo hilo kwa Rais Jakaya Kikwete, muda mfupi mara baada ya kuzindua jengo hilo leo.



Mkuu wa Kitengo cha Matibabu ya Dharula, Prof. Victor Mwafongo (kushoto), akifafanua jambo kwa Rais Jakaya Kikwete mara baada ya uzinduzi wa Jengo hilo la Emergency Medical Department leo.

Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, David Mwakyusa (katikati) wakipiga picha ya kumbukumbu na baadhi ya wahusika wa jengo la Shule ya Meno baada ya kukagua.
Baadhi ya Wauguzi wa Kitengo cha Matibabu ya Dharula, kutoka (kulia), Khadija Juma, Obeid Mgina, Mkurugenzi wa Kitengo hicho, Andrew Mziray na Mkuu wa Kitengo hicho, Victor Mwafongo, wakipiga picha ya kumbukumbu mbele ya Bango linalotambulisha jengo hilo mara baada ya uzinduzi wa jengo hilo leo.






No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.