Habari za Punde

*MAAFISA WA CIA WAUAWA AFGHANSTAN

Kundi la Taliban limedaiwa kuhusika na shambulio lililosababisha vifo vya maafisa wanane wa idara ya ujasusi ya Marekani CIA, huko nchini
Afghanistan. Shambulizi hilo limetokea katika kambi ya Kijeshi iliyopo Mashariki mwa nchi hiyo. Msemaji wa kundi la Taleban ambaye hakutaja jina lake amedai kuwa mpiganaji wa kundi hilo alijiunga na jeshi la
Afghanistan kwa lengo la kutekeleza mauaji hayo.
Hili ni shambulizi baya zaidi kuwakumba lililowakumba maafisa wa CIA tangu kuanza kwa vita nchini Afghanistan miaka minane iliyopita.
Shambulizi hilo limezua maswali kuhusu uwezo wa Majeshi ya Marekani kuweza kujilinda.
Katika tukio jingine siku ya jana Jumatano, bomu lililotegwa kando ya barabara nchini humo lilisababisha mauaji ya wanajeshi wanne raia wa Canada na mwandishi wa habari mmoja wa habari wa kike.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.