
Mashabiki wa bendi mpya ya Mapacha Wanne, wakielebuka Jukwaani wakati wa uzinduzi wa bendi hiyo uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Stereo Kinondoni.

Kahlid Chokoraa (kushoto) Jose Mara na Kalala Junior, wakiwa jukwani wakati wa uzinduzi wa bendi yao.

Kalala Junior (kushoto) akiwa na mpiga solo Shakashia wakifanya mambo jukwaani kuwapagawisha mashabiki wao.

Katika uzinduzi huo pia walikuwepo Banza Stone (wapili kulia) na Msafiri Diouf (wapili kushoto) nao wakiwasindikiza washkaji.

Banza na Diouf wakisalimia mashabiki jukwaani.

Jose Mara akimpagawisha shabiki wake jukwaani.


Msafiri Diouf, akipagawisha jukwaani.

Mashabiki wakimtunza Banza Stone alipopanda jukwaani kusalimia mashabiki na kuimba kwa hisia.

Huyu ni mpiga Tumba wa bendi hiyo akipagawisha kwa mipigo ya kipekee jukwaani.

Mtangazaji wa Star Tv, Saida Kilumanga (kushoto) akiwa na wasanii Bongo Flava na Dansi wakati akifanya mahojiano nao.

Msanii wa miondoko ya Bongo Flava, Mrisho Mpoto akiimba jukwaani wakati wa onyesho hilo.

Mashabiki wakiselebuka na misebene na Mapacha wanne ukumbini wakati wa uzinduzi huo.

Mrisho Mpoto akisalimiana na mashabiki waliofika kushuhudia onyesho hilo ukumbini.

Shabiki akimtunza ua Khalid Chokoraa wakati wa onyesho hilo.
No comments:
Post a Comment