"Huu ni msiba wa kitaifa, hivyo Taifa zima tutakuwa na maombolezo na bendera ya Taifa itapepea nusu mlingoti kwa siku saba"
Rais Jakaya Kikwete, akizungumza wakati alipokuwa akitangaza rasmi kuhusiana na kifo cha Simba wa Vita, Rashid Mfaume Kawawa, aliyefariki Dunia leo saa tatu na nusu asubuhi. Picha na (SPM)

Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (kulia) akiwa na Simba wa Vita, Rashid Kawawa, enzi ya uhai wao wakati walipomtembelea Mama mzazi wa Nyerere (kushoto) ambaye naye pia ni marehemu kwa sasa. Mungu aziweke roho zao peponi amina.

Rashid Kawawa, enzi za ujana na uhai wake, akiwa ofisini kwake akiendelea na kazi za kujenga Taifa.

Kawawa, watatu kutoka (kushoto) akiwa na baadhi ya Vingozi wa Chama cha Mapinduzi CCM, enzi za uhai wake katika moja ya shughuli za Kitaifa.

Kawawa hakuwa nyuma katika masuala mazima ya ukakamavu, pichani (watatu kutoka kulia) ni wakati alipokuwa na kikosi JKT, wakiwa katika mazoezi ya kivita kujiweka sawa.

Huyu ni Mmoja kati ya wakongwe wa Chama cha Mapinduzi, Kingunge Ngombalimwilu, akihojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na kifo cha Rashid Kawawa.

Hii ni picha ya mwisho ya uhai wa Rashid Kawawa, wakati Rais jakaya Kikwete (kushoto) alipomtembelea kumjulia hali wakati alipokuwa amelazwa kwenye Hospitali ya Muhimbili jana.

Kawawa (katikati) akiwa na mkewe (kulia) enzi za uhai wake katika moja ya shughuli zao.
No comments:
Post a Comment