Habari za Punde

*FEMA HIP WAANZA MKUTANO WA VIJANA DAR


Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk Makongoro Mahanga (kulia) akikata utepe kuzindua Mkutano wa Nne wa Vijana wa Femina HIP, ulioanza jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkurugenzi wa Femina HIP, Minou Fuglesang, (kushoto) ni Meneja Uhamasishaji Femina, Nash Molel.

Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk. Makongoro Mahanga, (watatu kushoto) akicheza na baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakiwakumbuka wanafunzi wenzao waliokufa kwa ajali ya moto katika Shule ya Sekondari ya Idodi Mkoani Iringa mwaka jana, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkutano wa Nne wa Vijana wa Femina HIP, ulioanza jijini Dar es Salaam jana, ambapo vijana hao walionyesha taa zinazotumia mionzi ya Jua ambazo zinafaa kwa matumizi ya wanafunzi kujisomea katika maeneo ambayo hayana umeme.














Kiongozi wa Bendi ya Mjomba, Mrisho Mpoto, akiimba na wanamuziki wake wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkutano wa Nne wa Vijana wa Fema HIP, uliozinduliwa na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana jijini Dar es Salaam . Mkutano huo ulioanza leo na utafanyika kwa muda wa siku tatu jijini ambapo umewakutanisha wanafunzi mbalimbali kutoka katika Mikoa tofauti.














Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Makongoro Mahanga (katikati) Mkurugenzi wa Fema Club, Minou Fulgesang (mzungu) na Mrisho Mpoto wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na baadhi ya walimu wa Club za Fema za wanafunzi, wakati wa uzinduzi wa mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.