Habari za Punde

*HABARI PICHA JIJINI DAR ES SALAAM LEO



WANAFUNZI WA GOBA WAHAHA NA USAFIRI, HUPANGA FOLENI KUINGIA KATIKA DALADALA KAMA WAFUNGWA...

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Goba jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye foleni ya kuingia katika usafiri wa Daladala aina ya Chai Maharage katika Kituo cha magari yaendayo Goba mwisho, kilichopo Mbezi Tang Bovu Mbezi Beach jana asubuhi. Wanafunzi hao wamekuwa wakilazimika kupanda maroli ya mchanga ama kuning’inia katika magari yaliyojaa kupita kupita kiasi kutokana na uchache wa magari na barabara mbovu, jambo ambalo husababisha ajali za mara kwa mara katika njia hiyo.

BIASHARA ISIYO NA tbs.........WABONGO BWANA..













Wafanyabiashara wa Utumbo wa kuchoma, (kulia) wakiwahudumua wateja wao eneo la Vingunguti Dar es Salaam jana. Pamoja na tishio la ugonjwa wa kipindupindu jijini lakini bado wafanyabiashara hao wanafanya biashara zao bila kufuata kanuni na taratibu za afya ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko.

WACHUUZI WA MBUZI DAR WALIA WATEJA HAKUNA....














Wafanyabiashara wa Mbuzi, Mohamed Nasor (kushoto) na Daniel Charles, wakikagua mbuzi wao ili kujua uzito kwa ajili ya kuuza kwa wateja wao (hawapo pichani) kama walivyokutwa na mpiga picha wetu jana kwenye Soko la Mbuzi Vingunguti Dar es Salaam. Mbuzi mmoja kwa sasa huuzwa Sh. 40, 000 hadi 50,000.

WASAJILI LAINI ZA SIMU WALALA USINGIZI KWENYE MABANDA YAO...DAR




















Wasajili laini za simu za mkononi, wa Mnyamani Buguruni Dar es Salaam, wakimsajilia mka



















No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.