Habari za Punde

*VODACOM YAZINDUA KAMPENI YA KUCHANGIA WALIOPATWA NA MAAFA

Mkurugenzi wa Kitengo cha Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Meja General, Bakar Shaban (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Dietlof Mare (katikati) na Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom, Ephraem Mafuru, na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom, wakituma ujumbe wa maneno kupitia simu zao za mkononi, ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Kampeni ya kuchangia waliopatwa na Maafa ambapo ujumbe mmoja unatozwa Sh. 250. Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika jijini Dar es Salaam. Ili kuchangia kupitia simu yako ndugu msomaji unatuma SMS yenye neno MAAFA kwenda katika namba 15599 na kila sms moja itatozwa Tsh. 250 tu ikiwa ni pamoja na VAT.

Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Kitengo cha Vodacom Faundation Maafa, wakipozi kwa picha wakati wa uzinduzi huo.

Sufianimafoto (kushoto) akiwa na baadhi ya wapiga picha wenzake wa Vyombo vya habari, Kutoka (kulia) ni Francis Dande wa Tanzania Daima, Albart Jackson wa Changamoto na Kassim Mbarouk wa Jambo Leo nao wakiwakilisha katika uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.