Ulijitolea kwa hali na mali maisha yako dada wananchi wameona umuhimu wako wa kuwa polisi wamekuzawadia pokea.....si hongo hii ni pongezi....
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (kushoto) akimkabidhi pesa Sh 100,000, Wp. Mwachum Haji, ikiwa ni pongezi baada ya kuwa mstari wa mbele wakati wa tukio la kuwakabili majambazi waliotaka kupora gari walioanza kurushiana risasi na Polisi maeneo ya Magomeni Kagera hivi karibuni. Katika hafla hiyo iliyofanyika jijini jana pia walipongezwa askari wote saba walioshiriki zoezi hilo walipongezwa kwa kukabidhiwa pesa kutoka kwa watu binafsi na makampuni mbalimbali.
Hongera dada umeonyesha ujasiri wa hali ya juu....

Huu ndiye Bonge Barabarani, akihum Haji, baada ya kukabidhi kitita cha Sh 100,000 kwa niaba ya Clouds Fm, ikiwa ni zawadi na pongezi kwa Polisi mwanadada pekee aliyekuwamo katika kupambana na majambazi waliotaka kupora gari. Picha Zote na (SPM)

Askari Polisi waliopambana na majambazi yaliyofanya jaribio la kupora gari hadi kuyaua, kutoka (kushoto), Mkuu wa kikosi Maalum (CRT), Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Inspector Kivumbi Kassim, Pc Mussa Ngunywai, Pc Ivan Jasson, Pc Arnold Kihaga, CPL Lucas Wagunja na CPL Hassan Mshindo, wakiwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati wa hafla ya kuwakabidhi zawadi kwa kazi nzuri waliofanya kupambana na majambazi, kuyaua bila kumdhulu raia.
No comments:
Post a Comment