Habari za Punde

*NDOA YA MAPACHA WALIOWAOA MAPACHA

"Oya Hebu mwangalie wa kwako vizuri usijejichanganya ukamfuata wangu bureee"

Ebwana kama Mayai hawa mapacha walivyofanana, hii ni ndoa iliyofungwa hivi karibuni jamaa hawa mapacha waliamua kuoa sehemu moja tena mapacha wenzao, eti walipuka kuchanganyana kwa mademu wengine wenye tamaa kutokana na jinsi walivyofanana. Na hata walipofika kuwachumbia mapacha wenzao nao pia walishukuru kutokana na wao pia hawakuwahi kuwa na rafiki wa kiume wakiogopa kuwachanganya kwa jinsi walivyofanana. Sasa ngoma ipo siku moja mmoja akasafiri na mwingine akafika kumtembelea mwenzake anaweza kuitwa jina anaoitwa pacha wake kwani imeelezwa hata mavazi wanayovaa ni sare kwa kila kitu hadi utembeaji wao na kuongea, je? kufanya hivi kutawaepusha na waliojaribu kuyakwepa??????

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.