Habari za Punde

*SAMAKI WA MAGUFULI WABAKI TANI 119 KUTOKA 299.3-1

Hiki ndicho chumba cha kuhifadhia samaki hawa mheshimiwa........Waziri Mkuu akionyeswa na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli, Chumba cha kuhifadhia samaki hao.

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli, (katikati) akimuonyesha Waziri Mkuu jinsi samaki hao wanavyopimwa wakati Waziri Mkuu uwa na ziara ya kutembelea Kiwanda hicho jana.

Hawa jamaa ni noma walikuwa wakituchukulia hadi vijisamaki hivi.........Hongera sana Magufuli..Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (wapili kushoto) akionyeshwa samaki wadogo ambao ni miongoni mwa samaki waliokamatwa katika meli ya uvuvi haram, wakati alipofanya ziara katika Kiwanda cha Samaki na kukagua vifaa vya uvuvi vilivyokamatwa ambavyo vipo kwenye Kituo cha Polisi cha Centre jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli, (katikati) ni Mkurugenzi wa Deep Fish Authority, Geofrey Nanyaro


Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania, (JWTZ) wakipakia samaki wa Magufuli kwenye gari lao kutoka kwenye Kiwanda cha samaki cha Mwenge Dar es Salam. Hadi jana jumla ya Tani 180 za samaki hao zimekwisha gawiwa kwa Taasisi mbalimbali kutoka Tani 299. 3-1.

Mmoja wa wafanyakazi wa Kiwanda cha samaki cha Mwenge, akikokota samaki kwenda kupima na kupakia katika magari yaliofika kiwandani hapo kuchukua samaki hao.




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.