Habari za Punde

*VODACOM YAZINDUA PROMOSHENI YA TUZO MILIONEA AWAMU YA PILI

Na SPM
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom, leo imezindua awamu ya pili ya Promosheni ya kubwa ya ‘Tuzo Milionea’, ambayo itamwezesha mteja wa Vodacom kujishindia Sh. Milioni 100 fedha taslim.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja Matukio na Promosheni wa Kampuni hiyo, Rukia Mtingwa, alisema kuwa katika Promosheni hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi mitatu, pia wateja wengine 90 watakaopata nafasi wataweza kujishindia muda wa maongezi wenye thamani ya Sh. Milioni 9.

Aidha aliongeza kuwa wateja wengine saba watashinda muda wa maongezi wa sh. 100, 000 kupitia Droo za wiki zitakazofanyika kwa kipindi cha wiki 12.

“Promosheni hiyo ni mwendelezo wa Promosheni ya Tuzo Milionea, iliyochezeshwa na Vodacom mwaka jana wa 2009, ambapo mshindi wa droo kubwa alikuwa ni Renatus Mkinga, mazi Ukonga Mombasa jijini Dar es Salaam” alisema Rukia.

Rukia alifafanua kuwa Promosheni hiyo ni kwa wateja wa malipo ya kabla na baada, ambapo mbali na droo za kila wiki pia kutakuwa na droo kubwa za kila mwezi zitakazowawezesha wateja wa Vodacom kushinda zawadi kem kem.

Naye mshindi wa Droo kubwa ya mwaka jana, Renatus Mkinga, akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo, aliwashukuru Vodacom kwa kuanzisha Promosheni hii, aliyoiita ni mkombozi wa maisha ya walalahoi kama yeye,ambapo kwa upande wake ameweza kufanya mambo makubwa kupitia kitita hicho alichoshinda kutoka Vodacom.

“Kwakweli nawashukuru sana Vodacom, kwa kuanzisha Promosheni hii ambayo mimi binafsi naona ndiyo mkombozi wa maisha yangu kwani nimeweza kujenga nyumba nzuri nay a kisasa na kununua gari la kifahari na kufanya mengi tu kupitia pesa hii, na sasa muonekano wangu mbele ya watu ni sawa na mheshimiwa fulani” alisema Mkinga.

Mknga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mafanikio aliyoyapata baada ya kuwa milionea wa Vodacom.
Mkinga akishuka kwenye gari lake baada ya kuwasili kwenye Hoteli mpya ya Double Tree, ulipokuwa ukifanyika mkutano wa uzinduzi wa Promosheni ya Tuzo Milionea awamu ya pili.

Mshindi wa Tuzo Milionea wa mwaka jana, Renatus Mkinga, akionyesha mafanikio yake (gari) alilonunua baada ya kukabidhiwa kitita cha Sh.milioni 100 mwaka jana.



Meneja wa Matukio na Promosheni wa Kampuni ya Vodacom, Rukia Mtingwa (kulia), Mkuu wa Idara ya Udhamini na Mawasiliano, George Rwehumbiza (katikati) na Meneja wa Huduna Bidhaa, Elihuruma Ngowi, wakionyesha mabango ya matangazo ya Promosheni ya 'Tuzo Milionea' awamu ya pili, iliyozinduliwa Dar es Salaam leo mchana. Picha na (SPM)



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.