Habari za Punde

*BENKI YA KCB YATOA MSAADA KWA KITUO CHA AFYA BUGURUNI DAR















Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa KCB Tanzania, ambaye pia ni Mbunge wa kuteuliwa, Janet Mbene (kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vifaa vya Hospitali vyenye thamanai ya Sh, milioni 4.3, Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni Kwa Mnyamani, Dar es Salaam, Mwajuma Mbaga, vilivyotolewa na Benki ya Biashara ya Kenya (KCB), leo mchana. Katikati ni Viongozi wa Kata ya Buguruni.














Muuguzi wa kituo cha Afya cha Buguruni Kwa Mnyamani, Sister Anna Mfanga (kushoto) akitoa huduma ya kumpima uzito mtoto, Idaya Omar, katika Kituo hicho wakati Benki ya KCB Tanzani ilipofika kituoni hapo na kutoa msaada wa vifaa vya Hospitali leo mchana. Kulia ni mama mzazi wa mtoto huyo, Rukia Mohamed.



Mkuu wa Masoko wa Benki ya Biashara KCB, Christina Manyenye, akicheza na mtoto Abdallahman Salum, wakati walipofika kwenye Kituo cha Afya cha Buguruni Kwa Mnyamani Dar es Salaam leo mchana na kutoa msaada ya vifaa vya Hospitali.

*MIUNDOMBINU MIBOVU JIJINI DAR ES SALAAM, Kawambwa watu watavunjika miguu, ohooo!
Mkazi wa jijini Dar es Salaam, akitoka kwenye shimo la kupitishia maji machafu baada ya kutumbukia kwa bahati mbaya. Shimo hilo limeachwa wazi kutokana na kuibwa mfuniko wake katika barabara ya Kivukoni, jambo ambalo ni hatari kwa watumiaji wa njia hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.