Mfanyakazi katika Duka la Viatu la Bata lililopo Mtaa wa Jamhuri Dar es Salaam, Gerard Kayanda (kushoto) akimjaribisha viatu mteja wake, Zakia Salum, wakati alipofika kwenye Duka hilo kununua viatu. Asilimia kubwa ya Viatu vianvyouzwa kwenye duka hilo ni ngozi halisi na bei ya kawaida anayoweza kumudu Mtanzania yeyote.
*Mandamano ya BAJAJI katikati ya mji Dar
Madereva wa Bajaji wakiandamana katika maeneo ya Posta Mpya Dar es Salaam leo mchana, wakati wakielekea katika msiba wa mwenzao, ambapo waliamua kupita katika maeneo ya katikati ya mji ili kuonyesha umuhimu wa usafiri huo uliokuwa umepakia abiria zaidi ya sita kila Bajaji moja.
*Marekebisho ya Nguzo za umeme....
Fundi wa Tanesco, akikwea Nguzo ya Umeme iliyopo Buguruni Sheli Dar es Salaam, akikata waya na kuondoa transifoma, kwa ajili ya kufanya marekebisho ya nguzo hizo zinazoondolewa na kufungwa nguzo za chuma.
*Wabunifu wa mavazi wachangia Elimu Wialaya ya Kisarawe.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Mwantumu Mahiza (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia mfuko wa Elimu Wilaya ya Kisarawe, uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Mbunifu wa Mavazi ambaye ni mdhamini wa harambee hiyo, Ally Rehmtullah, Mwenyekiti wa harambee hiyo, Profesa, Emmanuel Bavu na Mbunge wa Kisarawe, Athuman Janguo
*Wajasiliamali katika wimbi la mawazo juu ya biashara zao
Wafanyabiashara wa mayai, wakionyesha sura za uchovu wakati wakisubiri wateja katika Mtaa wa Kisutu Dar es Salaam leo. Trei moja kwa sasa huuzwa Sh. 6500 hadi 7000.
Wabeba mizigo wakipakia magunia yaliyosheheni Chupa Chakavu za Plastiki, kwa ajili kwenda kuuza, ambapo chupa hizo huyeyushwa na kutengenezwa bidhaa mbalimbali. Wakusanyaji wa chupa hizo huuza kwakilo kwa mawakala wanaonunua chupa hizo.
*Miundombinu mibovu Dar
Maji machafu yakiwa yametapakaa kwenye barabara iliyopo Mtaa wa Lybya Dar es salaam, na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa maeneo hayo ambao wameeleza kukelwa kwao na maji hayo yanayotoka katika jengo la ghorofa lenye makazi ya watu katika neo hilo.
No comments:
Post a Comment