Habari za Punde

*MARTINA CHAMBIRI WA MIAKA 5 ITALIA SASA KIDATO CHA 6 DAR














Martina Chambiri akiwa na Mama yake mzazi pamoja na baadhi ya wanafamilia, mara baada ya kupokea cheti chake wakati wa maafali ya kidato cha Sita cha Shule ya Sekondari ya Royola leo mchana.

"Hebu nikuwekee vizuri mwanangu eeeh!"














Mama mzazi wa Martina, Margaret Chambiri, akimrekebisha mwanae wakati wa maafali hayo.





Wanafunzi wahitimu wa Kidato cha Sita katika shule ya Sekondari Royola Dar es Salaam, Martina Chambiri (kushoto) akiwa na furaha wakati akipozi kwa picha na mwanafunzi mwenzake, Naima Zacharia mara baada ya kupokea vyeti vyao wakati wa maafali yaliyofanyika katika Shule hiyo leo.



Martina Chambiri, akipokea cheti cha kuhitimu kidato cha Sita.




Martina, akiwa na cheti chake mara baada ya kupokea, akiwa na furaha lukuki.






Martina akiwa na wenzake katika maafali hiyo.
Na Sufianimafoto Reporter
JE wamkumbuka msanii huyu? Huyu si mwingine ni Martina Chambiri aliyewahi kuwawakilisha watoto wenzake Watanzania, katika Tamasha la Wimbo wa Watoto lililofanyika huko nchini Itali mwaka 1995.
Katika Tamasha hilo Chambiri alishiriki akiwa na umri wa miaka 5, wakati huo akisoma darasa la awali (Chekechea) na alifanikiwa kushika nafasi ya tatu Kiduni na kushika nafasi ya kwanza kwa Afrika, kati ya watoto 18 walioshiriki tamasha hilo 11 kati yao wakiwa ni kutoka Italia na 7 Mataifa mengine baada ya kuimba wimbo wake wa Tanzania Eeeeeh, Tanzania Eeeeh.
Chambiri alianza elimu ya Msingi mwaka 1998 katika shule ya St. Costantine ya jiji Arusha na baadaye kumalizia elimu hiyo katika Shule ya St. Mary ya Mbezi Beach Dar es Salaam, hadi 2005 alipoanza elimu ya Sekondari katika shule ya Marian iliyopo Bagamoyo na hatimaye leo, alisimama mbele ya halaiki ya watu na kupokea cheti chake cha kuhitimu elimu ya Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Royola.
Chambiri ni miongoni mwa wanafunzi 229, waliohitimu katika shule hiyo jana.
Akizungumza na Mtanzania Jumapili mara tu baada ya kupokea cheti chake, alisema kuwa anajisikia furaha zaidi na hasa baada ya kuhitimu huku akiwa na ndoto za kuendelea na elimu ya juu ya Chuo Kikuu na kuendeleza kipaji chake cha Sanaa hususan kuimba.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.