Habari za Punde

*MATUKIO YA WIKI DAR KATIKA PICHA

*JERRY MURO NA WENZAKE WAPATA DHAMANA........















Jerry Muro, akiwa kwenye gari mara baada ya kupatiwa dhamana, akiongea na mmoja wa watu waliokuwa wakishughulikia dhamana yake.














Mmoja wa washitakiwa katika kesi ya Rerry na wenzake, Edmund, akipanda katika gari nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kupata dhamana.
















Edmund, akipunga mkono nje ya Mahakama hiyo kwa raia waliokuwapo Mahakamani hapo wakifuatilia kesi hiyo.














Baadhi ya waanishi wa habari wakiwa kwenye Mahakama hiyo wakifuatilia kesi hiyo huku kila mmoja akiwa bize ili kunasa kila tukio linalojiri mahala hapo.





















Waandishi wakiwa bize kwenye mlanga wa chumba cha Mahakam, ilipokuwa ikisikilizwa kwa mara ya kwanza Kesi inayomkabili mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji la Tanzania, TBC1, Jerry Moro na wenzake.





















Jerry na wenzake wakiwa katika Chumba cha Mahakama wakisomewa mashitaka yanayowakabili.




















Jerry Muro akitoka kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar jana mara baada ya kupatiwa dhamana na wenzake.




















Huyu jamaa, inaonekana alikuwa hajiamini kwani baada ya kutoka nje ya Mahakama hiyo, alianza kutimua mbio bila kituo hadi alipofanikiwa kuwaona nduguze waliompeleka kwenye gari.


























Mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC, Jerry Muro, akiwa chini ya ulinzi wakati akirejeshwa katika Chumba cha Mahabusu, wakati akisubiri kukamilika kwa taratibu za dhamana katika kesi inayowakabili ya kula njama ya kuomba rushwa ya Sh Milioni 10 na wenzake, Edimund Kapama na Deogratias Mgassa, katika Mhakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam.

*TOT PLUS WAKABIDHIWA VYOMBO VYA MUZIKI VYA TSH. MILIONI 100...

















Mweka Hazina wa Chama cha Mapinduzi CCM, Amos Makala (katikati) akipiga Drams ikiwa ni ishara ya kukabidhi vyombo vipya kwa bendi ya TOT Plus, vyenye thamani ya Sh, milioni 100. Kushoto ni Mkurugenzi wa bendi hiyo, John Komba, (kulia) ni mratibu wa bendi hiyo, King Dodoo.

















Mweka Hazina wa Chama cha Mapinduzi CCM, Amos Makala (katikati) akipiga tumba ikiwa ni ishara ya kukabidhi vyombo vipya kwa bendi ya TOT Plus, vyenye thamani ya Sh, milioni 100. Kulia ni Mkurugenzi wa bendi hiyo, John Komba, (wapili kushoto) ni mmoja wa waimbaji wa kundi la Taarab la TOT, Khadija Kopa, (kushoto) ni mratibu wa bendi hiyo, King Dodoo.
















Wanamuziki na wanenguaji wa bendi hiyo wakipozi katika picha ya pamoja wakati w

















Fundi mitambo wa bendi ya TOT Plus, Said Makeke, ajaribu kurekebesha vyombo hivyo wakati wa hafla ya kukabidhiwa vyombo hivyo vyenye thamani ya sh. milioni 100.

*BOMU LATIKISA DAR, WAKAZI WA MSASANI HOFU TELE...

























Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ, Koplo PatricKijuo, akiwa na bomu linalodhaniwa kuwa na uzoto wa takriban Kg 13, baada ya kuliondoa kwenye nyumba iliyopo Mtaa wa Msasani Mandazi Road Dar es Salaam jana, ambako liliwekwa na kijana aliyeelezewa kuwa alikuwa akizunguka nalo huku kutafuta wateja kama chuma chakavu kwa wakazi wa mtaa huo bila mafaniko na kuamua kudampo katika nyumba hiyo, jambo ambalo lilizua hofu kwa wakazi wa eneo hilo hususan wanaoishi katika nyumba hiyo ambao walihama nyumba yao kwa muda.



















Wakazi wa Msasani, wakilizonga gari la jeshi lililobeba bomu hilo, mara baada ya kuondolewa kwenye nyumba ya Michael Jacob.
















Wataalam wa mabomu, Meja Mchomvu (kulia) na Luteni Mbewa (katikati), wakimuonyesha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa kinondoni, Elias Kalinga, Bomu lililoondolewa kwenye nyumba ya Michael Jacob, eneo la Msasani Mandazi Road Dar es Salaam.

















Askari huyo akiliweka bomu hilo kwenye gari la Jeshi lenye namba za usajiri JWTZ 2632, ambalo liliondoka na bomu hilo.






































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.