Habari za Punde

*SERENGETI WAANGUSHA BONGE LA PARTY KUWASHUKURU WAANDISHI WA HABARI DAR















Wasanii wa kundi la Wanne Stara, wakionyesha umahiri wao wa kujikunja katika mchezo wa Yoghat, wakati wa Sherehe ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Msasani Beach Club jana usiku.










Mgeni Rasmi katika sherehe hiyo, Seif Khatib (katikati) akiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Serengeti, wakati akiingia ukumbini kufungua rasmi shererhe hiyo.










Mgeni rasmi, Seif Khatib (wapili kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Serengeti, Mark Bomani (kushoto) na Maeneging Director wa Tanzania Daima, Kibanda, wakikata keki kwa pamoja kuashiria kufungua rasmi sherehe hiyo jana. Kulia ni Managing Director wa Serengeti, Teddy Mapunda, akisherehesha hafla hiyo.








Wakipozi katika meza yao huku wakifurahia burudani iliyokuwa ikiendelea mbele ya macho yao.




Sufianimafoto (kulia) akipozi kwa picha na Full Shangwe (kushoto) na Teddy Mapunda, ambaye ni mdau mkubwa wa Blogs za washkaji hawa na wengine.





Wanenguaji wa bendi ya Akudo Impact, wakishambulia jukwaa wakati wa sherehe hiyo, kuwapagawisha waandishi wa habari waliofulika lukuki katika ukumbi huo.

Mhariri wa gazeti la Changamoto, (kushoto) akipokea cheti ikiwa ni ishala ya kuonyesha mchango wa gazeti hilo kwa Kampuni ya Bia ya Serengeti.









Sufianimafoto (wapili) kulia, akipozi na wamiliki wenzake wa Blogs, mara baada ya kutunukiwa Vyeti na Kampuni ya Bia ya Serengeti katika sherehe hiyo kwa kuitangaza vyema na kufanya kazi na kampuni hiyo kwa kipindi kirefu. Kutoka kushoto ni Fullshangwe, Issamichuzi, Mohameddewj blog na (kulia) ni Michuzi Junior, wote wakiwa na furaha tele.








Huyu ni Bonge barabarani, akipokea cheti kwa niaba ya Clouds Redio, wakati wa sherehe hiyo.









Baada ya zawadi na mlo wa usiku 'Dinner' ilikuwa ni sesion ya muziki, ambapo mgeni rasmi alifungua muziki sambamba na Teddy Mapunda wa Serengeti na hatimaye misebene ikaanza kwa wote mpaka kuchweeeeeeeee.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.