Habari za Punde

*MISS TANZANIA 09 ATUPWA SEGEREA, APANDA KARANDINGA




JINAMINI limezidi kuwaandama warembo wanaotwaa taji la Miss Tanzania, kwa kufanya vitendo vya kuvunja sheria na kujikuta wakitupwa Selo, na safari hii ni zamu ya Mrembo aliyetokea jijini Mwanza na kuwamwaga warembo lukuki kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania, na kutwaa taji hilo la Miss Tanzania 2009, Miriam Gerald (22), aliyekwenda Segerea leo bila kuaini macho yake.
Ilikuwa ni mida ya saa tatu na robo, askari polisi walipoizingira nyumba ya Kenedy Victor, ambaye ni rafiki wa kiume wa Miss Tanzania 2009, Miriam Gerald, iliyopo maeneo ya Mikochezi Dar es Salaam leo asubuhi na kuwakamata wapendanao hao waliotoka ndani huku wakifikicha macho kuashiria ni watu waliochoka kwa usingizi mzito na kuwafikisha kwenye Kituo cha Polisi cha Oysterbay.
Baada ya kufikishwa katika Kituo hicho walipandisha kwenye gari dogo lililokuwapo kituoni hapo nakupelekwa kwenye Mahakama Wilaya ya Kinondoni na kusomewa mashitaka yanayowakabili, ya Kujeruhi na kuharibu mali yenye thamani ya Sh. 720,000.
Akisoma mashitaka hayo, mbele ya Hakimu Kuye Rusemwa, mwendesha mashitaka, PP, Nasor Sisiwaya, alisema kuwa washitakiwa hao siku ya tarehe 5 mwezi huu majira ya saa 1: 40 usiku, huko maeneo ya Mikocheni, washitakiwa walimpiga kwa kitu chenye ncha kali na kumjeruhi mlalamikaji, Shabani Moshi.
Mbali na hilo pia waliharibu Vifaa vya muziki, mali ya mlalamikaji huyo wakiwa katika eneo hilo la Hoteli ya Peace Of Mind, ambapo ilidaiwa rafiki huyo wa kiume wa Miriam, alichukua gitaa na kulivunja kwa kutumia goti lake.
Baada ya kusomewa mashitaka hayo waliingizwa lupango huku baadhi ya ndugu wa kidume Kenedy, wakihaha huku na huko kuhangaikia dhamana bila mafanikio.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi Februari 25 mwaka huu na washitakiwa walipanda Karandinga kuelekea Segerea baada ya kukosa wadhamini waliotimiza vigezo vya dhamana.


MAMBO YALIKUWA HIVI MAHAKAMANI HAPO.














Askari polisi akilikimbiza Karandinga lililombeba Miss Tanzania 09, wakati likitoka kwenye lango la Mahakama ya Wilaya Kinondoni ili apande.

"Duh! Kimasikhara nakwenda Segerea, wala siamini sijui kwa nini sikumtaarifu hata Lundenga, angenisaidia kunidhamini".........





Miss Tanzania 2009, Miriam Gerald, akiwa chini ya ulinzi wa Askari Polisi wakati akisindikizwa kuingia Chumba cha Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam leo. Miriam alifikishwa Mahakamani hapo na rafiki yake wa kiume (Boy Friend) aliyetambulika kwa jina la Kenedy Victor, kwa kosa la kujeruhi na kuharibu mali yenye thamani ya Sh. 720, 000, hata hivyo washitakiwa hao walipanda Karandinga kuelekea Segerea baada ya kukosa wadhamini wenye kutimiza vigezo vya dhamana.
"Duh! kumbe waandishi wananisubiri? mbona wakati naingia hawakuwepo? yaani na baba keshajua sasa".....
















Miriam akiwa chini ya ulinzi..
"Afande basi naomba utupe angalau muda na simu yangu ili niwapigie ndugu zangu waje kutudhamnini"















Miss Tanzania 09, Miriam Gerald akiwa na Boy Friend wake, Kenedy Victor, wakati walipokuwa kwenye chumba cha Mahakama ya Wilaya Kinondoni.

"Duh! wamenitoa ndani tena wananirudisha?, nilidhani ndo nimedhaminiwa niende home"














Miriam akirejeshwa ndani ya chumba cha mahabusu baada ya kukosa wadhamini.

"Ebwana eeh! wala siamini yaani napanda Karandinga? Icheki hii mijamaa inavyonicheki sijui itanifanyi"?


















Kenedy Victor akipanda Karandinga kuelekea Segerea, baada ya kukosa dhamana.
"Nimewakomesha nimejifunika sura hamnioni ng'ooooo"



Miss Tanzania, akipanda Karandinga huku akiwa amejifunika khanga ili kuficha sura, jambo ambalo halikumsaidia kitu kwani tayari alishanaswa na kamera za waandishi wote waliokuwapo Mahakamani hapo wakati akiingia akiwa na kibalauzi cha kinyumbaninyumbani.




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.