Habari za Punde

*ASHANTI YAZINDUA KLABU YA NGUMI




Na Mwandishi Wetu, jiji Dar es Salaam
KLABU ya Ashantia jijini Dar es Salaam, imezindua Klabu mpya ya ngumi
kwa ajili ya kuendeleza mchezo huo kwa vijana wanaopenda masumbwi.
Klabu hiyo yenye maskani yake Ilala, imezinduliwa hivi karibuni katika
Ukumbi wa CCM Ilala Boma, na kuhudhuliwana mashabilki lukuki wa mchezo
huo waliojitokeza kwa ajili ya kushuhudia wanamasumbwi waliofuzu kuingia
katika Klabu hiyo wakionyesha umahiri wao wa kucheza.
Akizungumza mara baada ya kufanya uzinduzi huo kocha mkuu wa klabu hiyo
Rajabu Mhamila 'Super D' alisema klabu yake imezinduliwa kwa mafanikio
huku baadhi ya wakongwe wa mchezo huo wakijitokeza kushuhudia
mipamabano kadhaa kutoka kwa mabondia chipukuzi wa klabu za Ashanti na
Simba.
Alisema utambulisho huo uliokuwa chini ya Taasisi ya Kinyogoli Foundation,
ulishuhudia klabu yake yenye mabondia tisa ikitoka sare na wale wa Simba
huku kila moja ikifanikiwa kushinda michezo mitatu huku wakongwe wa mchezo huo, Koba Kimanga na Iraki Hudu wakitoa sapoti kwa vijana hao.
Alisema katika michezo hiyo ambayo kila timu iliwakilishwa na mabondia sita
ilishudia mabondia hao wakionyesha mchezo wa kusisimua huku mashabiki
wengi waliojitokeza kushudia wakimwaga sifa za pekee kwa
kocha Super D kwa kuwawezesha vijana kujipatia ajira.
Aliwataja mabondia waliopanda katika mchezo kuwa Abuu Mtamwe wa
Simba akipanda na Iddi Ramadhani katika uzito wa Bantam, Musa Shuza
akicheza na Bariki Manyota katika uzito huohuo, wakati Issa Dachi akipanda
na Badru Hassan katika uzito wa light weight.
Wengine ni Shaban Kipara aliyezichapa na Abjerina Kadri katika uzito wa
middle weight huku Issa Kimanga na Yahaya Athumani wakipanda katika
uzito wa super middle huku Salim Kindondi akipanda na Ibrahim Class katika
uzito wa light weight.
Alisema katika uzinduzi huo pia walizialika klabu za Vingunguti ambayo
haikutoa mchezaji hata mmoja huku ile ya amana ikipeleka mchezaji mmoja
wakati hizo zote zilitakiwa kupeleka wapiganaji watatau ili kuongeza hamasa
kwa washiri na kuongeza upinzani.
Pia Super D alisema katika uzinduzi huo moja ya mwanamama Halima
Kaubanika alijitokeza kutoa sapoti yake katika uzinduzi huo ambapo alitoa
ngrops seti moja na kuhaidi kutoa vikinga mdomo tisa huku akiwaomba
wadau mbalimbali kujitokeza kuunga mkono juhudi za kocha huyo katika
kukuza michezo wilayani Ilala.
Super D aliongeza kuwa baada ya kufanikiwa kuzindua klabu yake kwa hivi
sasa anajipanga kuiombea nafasi ya kushiri klabu bingwa ya ridhaa ya mkoa
wa Dar es Salaam kwa Shirikisho la mchezo huo nchini.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.